Zifahamu Aina Tofauti za Uvaaji Hijab

Wadada wengi wamekuwa wakitaka au kutamani sana kuvaa kwa kujistiri lakini wengine unakuta kuwa ili avae kiremba inabidi siku hiyo apange safari na kwenda kwa dada au mama mkwe ili aweze kumfungwa kiremba.

hakuna asiependeza katika vazi hili ingawa watu wengi wanasema kuwa ni rasmi kwa ajili ya wasichana wa kiislamu, lakini pia kama unataka kujistiri ni vizuri kuvaa kiremba tu ili kuleta muonekano mzuri na wenye heshima pia.Hivyo angalia hapa style za kufunga kiremba hiki.

 

Fahamu Faida za Manjano Katika Urembo

Manjano ni moja ya kiungo kinachotumika  katika mchuzi lakini pia imekuwa ikitumiwa a warembo kuweka ngozi katika hali ya usafi zaidi.Kwa wanaotaka kutumia ama urembo uwa na faida zifuatazo :-

  • Hutibu chunusi– Manjano ina ‘antiseptic’ na ‘anti-bacterial’ ambazo husaidia kupambana dhidi ya chunusi na vidonda usoni na kukupa muonekano mzuri. Manjano pia husaidia kupunguza mafuta usoni kwa wale wenye nyuso zenye mafuta.

Vinavyohitajika

  • Liwa kijiko kimoja cha chai
  • Manjano kijiko kimoja
  • Juisi ya limau

Changanya viungo hivi pamoja na kisha uipake usoni na ukae navyo kwa muda usio pungua dakika 10. Ili kuondoa chunusi, changanya manjano na maji safi kisha upake usoni na ukae hivyo kwa dakika 15 kabla ya kunawa uso wako kwa maji ya fufutende.

  • mask kwa wenye nyuso zenye mafuta mengi– Manjanoina manufaa katika ngozi zenye mafuta na husaidia kupunguza mafuta na hio upelekea kupunguza chunusi usoni.

Vinavyohitajika

  • juisi ya machungwa
  • liwa
  • manjano

Vichangaye vyote hivi kisha vipake usoni na ukae navyo kwa dakika kati ya 10-15 kabla ya kuosha.

  • Mask kwa ngozi kavu– Kama una ngozi kavu, unaweza kutengeneza ‘mask’ kwa kuchanganya ute wa yai moja, mafuta ya mizeituni vijiko viwili vya chai, namanjano vijiko viwili. Mchanganyiko huu unaweza kutumia kwenye ngozi kavu kama vile usoni, shingoni, magotini. Ukishajipaka ni muhimu uache kwa dakika 15 au 20 kabla ya kunawa.
  • Huondoa makunyanzi– Manjanoikichangaywa pamoja na viugo vingine ina ufanisi katika kuondoa makunyanzi usoni. Unaweza kuandaa mchanganyiko kwa kuchanganya unga wa manjano pamoja na mchele uliosagwa, maziwa na juisi ya nyanya na kupaka usoni na shingoni.Muda wa nusu saa ukishapita, unashauriwa kutumia maji moto kujiosha. Ukifanya hivi angalau mara moja kwa wiki uso wako utaanza kung’aa.
  • Kuondoa michirizi (stretchmarks)Manjanohusaidia kufuta michirizi. Changanya manjano na maziwa au maji kisha upake katika sehemu yenye michirizi. Baada ya dakika 30, oga kwa maji ya fufutende kisha upake losheni.

 

  • Faida ya manjanokwenye nywele –Manjano husaidia katika ukuaji wa nywele, pia kuondoa mba. Changanya manjano na olive oil kisha upake kichwani na ukae hivyo kwa dakika 30 kabla ya kuoga. Mchanganyiko huu ukiongezwa asali pia hupunguza kukatika kwa nywele.

 

 

Mambo ya Kuzingatia Katika Kuchagua Nguo za Ujauzito.

Imekuwa ikizoeleka kuwa endapo mama ni mjamzito basi nguo kubwa atakayo kuwa akivaa ni magauni na kujifunga kanga tu, lakini kumbe sio hivyo,  Dunia inabadilika na ulimwengu wa fashion unazidi kuendelea hivyo watu kama hawa nao wanapaswa kuonekana tofauti na kuendanana na fashion  sio kwa sababu tu ha hali yake.

Hata Hivyo wao pia mabao wamekuwa wabishi na kutaka kuendana na fashion bila kuwa na uchaguzi mzuri wanguo kulingana na hali yao, kwa mfano nguo za kubana sana, viatu virefu sana hii inamuumiza mtoto m, mara nyingine mama mwenyewe lakini pia unaweza kuonekana wa ajabu zaidi kwa sababu unashindwa kuzuia hisia zake kuendana na fashion.

Katika kuchagua nguo nzuri za wakati wa ujauzito unaakiwa kwanza:-

Kulikubali umbo lako.

kadri tumbo linavyokuwa na umb lako linaongezeka hivyo unapswa kutambua kuwa umbo lako sio kama pale mwanzo hivyo hata nguo zako zinabidi kuendana na hilo, nunua nguo ambazo hazibani , zenye kupitisha hewa kwa uraisi zaidi .

Usibadilishe mtindo wako wa kawaida.

kama ulikuwa unapendelea sana kuvaa magauni haina haja ya kubadilika kwa sababu ya hali yako ya ujauzito na kuanza kuvaa nguo zingine, angalia tu kuwa kama ni jinsi au sketi ndio umezoea kuvaa basi tafuta zile zenye kuipa nafasi hali yako na sio kubadilika kabisa.

Nunua vifaa vya mitindo.

Achana na habari ya kubwetea tu na kuonekana wa kawaida sana, vaa na nunua vitu kama hereni, bangili, saa na vitu mbalimbali vya mitindo na mapambo kupendezesha  muonekano wako.

Nunua nguo za rangi.

Kuna nguo ambazo zinatoa mwanga mzuri kwa mama mjamizto kwa kuzingatia pia na hali aliyonayo, jaribu kununua nguo zenye rangi ya kungaa ili kuonekana mrembo zaidi.

KUMBUKA:-Kuwa mjamzito sio mwisho wa kuwa mrembo, wengi wamekuwa wakijiweka kihasara hasara kwa sababu ya hali zao , Urembo wa mwanamke ni muda wowote  na hii inaendelea hata baada ya kujifunga na wakati wa kunyonyesha.

 

Makosa Wanayofanya Wanawake Katika Utumiaji wa Vipodozi na Urembo.

Kama ilivyo kote Duniani,  kuna makosa yanayofanywa kwenye kutumia vipodozi  kwa wanawake Tanzania. Ila kwa sababu tunapenda urembo na tuko kwa ajili ya kusaidiana ni bora kuyaona makosa hayo,yafuatayo ni makosa 10 ya kuweka vipodozi na jinsi ya kuzirekebisha.

 Nyusi

Kuna tabia ya wanawake kunyoa nyusi zao sana, na wengine kuzitoa kabisa. Alafu, wanaishia kuzichora na rangi nyeusi.

Hii inamfanya mwanamke kuonekana kama kikatuni, hivyo basi kitu cha kufanya ni:-

  • Badala ya kunyoa nywele zote, zipunguze kwa kiasi kidogo
  • Usituimie rangi nyeusi kuzijaza. Tumia rangi ya brauni
  • Kwa muonekano wa kiasili zaidi, tumia nyusi, poda ya nyusi au gel badala ya penseli.

Tumia faundesheni inayofanana na rangi ya ngozi yako

Ingawa kupata faundesheni inayofanana na ngozi yako ni ngumu, hasa kwa wanawake weusi zaidi, wanawake wengi wanapata shida na kukubali rangi ya kiasili na wanajaribu kutumia vipodozi kubadilisa rangi yao, hivyo ni bora kwanza :-

  • Kubali rangi yako ya kiasili
  • Rangi yetu inaweza ikawa mweusi au mweupe zaidi kutegemea na msimu. Kwa hiyo ni bora kuwa na faundesheni inayoendana na mabadiliko  hayp

 Usitumie poda asana

Wadada wengi wamekuwa wakihisi kwamba kutumia poda nying ndio kupendeza zaidi. Matokeo yake, wanaishia kuwa vituko tu , hapa unashauriwa :-

  • Tumia poda inayofanana na ngozi yako
  • Usiweke poda nyingi. Kiasi kidogo kitakutosha

Matumizi ya  kope bandia 

Wanawake wengi wanatumia kope bandia zisizo na ubora. Matokeo yake wanafanana na dolli ya mtoto.

Suluhisho:

  • Badala ya kutumia kope bandia, nunua wanja nzuri inayonyoosha na kunenepesha kope zako
  • Nunua kope bandia zenye ubora (zilizotengenezwa na nywele za binadamu au yalisan.

 Eyeshadows

Wanawake wanatumia eyeshadow zinazo ng’aa au za rangi kali. Zaidi ya hapo, hawazichanganyi vizuri.

Suluhisho:

  • Tumia eyeshadow za rangi ya dhahabu, brauni  au zambarau
  • Jifunze jinzi ya kuweka eye shadow vizuri, zikiwemo
    • Rangi ya highlighter ya kuweka chini ya nyusi zako
    • Rangi ya mpito
    • Rangi kuu ya eye shadow

 Mdomo

Kabla ya kuweka lipstick, hakikisha mdomo yako inaunyevu. Hii ni muhimu sana kwa lipstick yako kuseti vizuri.

Usiweke vipodozi kwa fujo

Kwenye swala la vipodozi, kutumia kidogo ni bora kuliko kutumia nyingi. Unataka urembo wako wa kiasili kuboreshwa, sio kubadalika kabisa.

Kwa kifupi, ukitumia vipodozi lakini unaonekana kama vile hujatumia vipodozi, basi hapo ndio utakuwa umepatia.

 

Urembo Kipindi cha Ujauzito na Baada ya Kujifungua.

Kipindi cha ujauzito wanawake wengi hujikuta wakiwa katika hali ya  kuchakaa kwa sababu ya hali zao.wengine ujikuta wakijiendekeza hata kufikia hatua ya kukatwa nywele au kutovaa vizuri kisa tu yeye ni mama mlezi wa mimba.Ukweli utabaki kuwa  sifa kuu ya mwanamke ni kuonekana msafi nadhifu na mwenye kuvutia siku zote.

Hali  hii ya kutokuwa nadhifu uweza kuendelea hata baaada ya kujifungua tena huku uweza kuwa mbaya zaidi kwa sababu mama anakuwa yuko busy sana na mtoto na hapaswi kupaka baadhi ya vitu vinavyoweza kumuathiri mtoto wake.

Mimba au mtoto haiwezi kuwa sababu kubwa ya mama kutokuwa mrembo, jukumu kubwa ni kubaki na muonekano wake ule ule wa zamani na ikibidi kuzidisha kwa sababu ni sifa ya kike.lakini urembo huu unapaswa kuzingatia zaidi upakaji wa mafuta au vipodozi ambavyo havina kabisa kemikali au harufu mbaya kwa mtoto anayemnyonyesha.

Kuna baadhi ya mazoezi pia yanaweza kusaidia kurudisha urembo na umbile lako lisizidi lilivyokuwa hapo awali, pia zingatia kula vyakula vya wastani kwa sababu wazazi wengi hujikuta wakijiachia na kula hovyo kwa kisingizio cha kuwa wananyonyesha.

Jaribu kuwa na nywele safi  ambazo  hazitakuwa zikimsumbua mtoto wako lakini pia pia usiwe unatumia muda mwingi kwenda saluni na kusababisha kukosa muda mwingi wa kukaa na mtoto kwa kipindi hicho, kwa upande wa kucha hakikisha kucha sio ndefu na usipende kupaka rangi kwa sababu wewe unatoa huduma kwa mtoto.

Kitu kikubwa cha kujitahidi ni kulinda muonekano wako wa ndani na wa nje na sio kuzaa kukufanye ubadilike uwe mtu mwingiene kabisa asiyejipenda na kujijali hata kidogo.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.