Hamisa Nae amjibu Diamond Kwa Hili.

Baada ya mwanamuziki  Diamond platinumz kutoa dongo kwa mwanamke aliyewahi kuwa nae katika mahuisano  Hamisa Mobeto kwa kumwambia kuwa anajua bado anamtamani lakini akae mbali nae kwa sababu mwili wake unapendwa na wengi atapata stress , Hamisa nae kaamua kumjibu Diamond kwa kejeli.

katika maneno hayo ambayo Hamisa alijionyesha kama anaimba wimbo flani lakini anatuma ujumbe kwa mwanaume huyo anasema kuwa Diamond alishindwa kumtunza kama mwanaume mwenye pesa na kwamba mapenzi yaliziwa na maisha na ndio maana iliwabidi waachane,

hukua na uwezo wa kunitreat kama millionaire, mapenzi yakazidiwa na maisha and we had to break somewhere,….sikuamini maneno yako na sikupenda the way they sounded,,wala aahadi zako hazikufikia what i wanted..

Hayo ni majibu baada ya diamond kumkshifu na kumwambia kuwa hawezi ku-handle stress za wanawake wengine kwa sababu yeye anapendwa na wengi.

Hamisa Ashauriwa Kuacha Kutumia Familia ya Diamond Kupata Kiki

Moja ya watu wa karibu wa familia ya Diamond platinumz amefunguka na kusema kuwa kwa sasa familia ya diamond imeshagundua kuwa Hamisa amekuwa akitumia jina la familia hiyo kwa ajili ya kujipatia kiki yake na muziki wake hivyo na wao kwa sasa wameamua kukaa kimya bila kumzungumzia mwanadada huyo.

Akiongea na moja ya waandishi wa kurasa za Udaku, mwanafamilia huyo anasema kuwa kwa sasa familia hiyo imegundua kuwa muziki wake hauendi kama asipowata au wao kumtaja mwanadada huyo na ndio  maana hata familia hiyo akiwepo esma, mama dangote na hata zari mwenyewe hawataki kumpa kiki tena.

Akimalizia kwa kuongea hayo anasema kuwa anchomshauri hamisa kwa sasa ni kufanya kazi kwa nguvu zote kwa sababu kama jina ameshalipata kutumia jina la diamond na anatakiwa kuakza buti.

Hamisa Amtupia Diamond Dongo Kuhusu Uchawi

Ni siku kadhaa zimepita tangu Hamisa alipatwa na skendo ya kumloga Diamond na kuvuja kwa sauti za Hamisa akiongea na waganga ili waweze kumtengeneza Diamond ili aweze kuijali familia yake na kumjengea nyumba.

Diamond alilalamika sana kuhusu swala hilo na baada ya hapo Hamisa alikiri kuwa ni kweli sauti ilikuwa ni ya kwake lakini hakuwa anamloga bali alikuwa anaongea na shekhe na kumuelezea matatizo ya mahusiano yake ili aweze kufanyiwa dua.

katika pitapita na kukutana na comments moja ya hamisa akimjibu shabiki yake kuhusu  maswala ya uganga na uchawi ambapo  kwa jinsi hamisa alivyojibu inaonekana kuwa dongo hilo lilikuwa linamlenga mzazi mwenzie huuyo kwa sababu Diamond ndio aliekuwa akilalamika baada ya kusikia kuwa Hamisa alikuwa akitaka kumloga, katika comments hizo,mambo yalikuwa hivi  ;-

MWANAUME KULIA MITANDAONI ETI UNALOGWA HUO NI  UMAMA, MWANAUME UNATAKIWA USEME BEIBY ONGEZA KUNILOGA NIKUONGE DUNIA” ambapo hiyo ilikuwa ni maoni ya shabiki na Hamisa alijibu  “TENA KUSEMA ONGEZA KUNILOGA NI UMAMA UNATAKIWA UWE MGANGA ILI KWENDA SAMBAMBA.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.