Hii Ndio Sababu Kubwa Iliyomfanya Happiness Kuficha Sura Ya Mwanaye

Miss Tanzania mwaka 2001 Happiness Magesse au maarufu kama Millen amefunguka na kuweka wazi sababu kubwa iliyomfanya mpaka akachelewa kuweka wazi sura ya mtoto wake King Kairo.

Millen alijifungua mtoto wake mwaka jana mwezi July lakini amemuonyesha mtoto wake mwaka huu mwezi wa machi ambapo alimficha sura yake kwa muda wa miezi tisa.

Wiki iliyopita Millen alianika sura ya mwanaye King Kairo kwa mara ya kwanza mtandaoni alipokuwa ametokea kwenye jarida la ‘Genievieve’ la nchini Nigeria.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo, Millen ameweka wazi kuwa sababu pekee iliyomfanya akamficha mtoto wake ni kutaka amuonyeshe katika muda sahihi na katika kipindi hiki au mwezi huu wa maadhimisho ya ugonjwa wa Endometriosis ambao umekuwa ukimsumbua kwa miaka mingi.

Nilikuwa na mpango ambao ulikuwa una muda sahihi, mtoto wangu ni sehemu kubwa ya stori yangu ya maisha yangu hivyo nilihitaji kumuonyesha during Endometriosis month mwezi huu machi”.

 

Tazama Picha Ya Kwanza Ya Mtoto wa Happiness Megese

Aliyekuwa Miss Tanzania 2001 Happiness Magesse ama maarufu kama Millen Magesse katika ulimwengu wa fashion ameweka hadharani picha ya kwanza ya mtoto wake King Kairo.

Happiness alimkaribisha mtoto wake wa kwanza tarehe 21 mwezi wa saba mwaka jana lakini mpaka King kairo anafikisha miezi nane alikuwa hajaweka picha yake mtandaoni mpaka jana.

Happiness na King Kairo

Happiness amekuwa muwazi na kipindi kigumu alichopitia mpaka kumpata mtoto huyo hasa kwa sababu anasumbuliwa na ugonjwa unaoitwa Endromittiosis ambao ulikuwa unampa wakati mgumu kupata mtoto.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.