Hussein Machozi aeleza kwanini yeye huadhibu mtu yeyote amtukanaye kwenye mitandao wa kijamii

Tofauti na Ali Kiba ama ata Diamond ambao wamezoea kutukanwa mitandaoni bila kuchukua hatua yoyote, Hussein Machozi hawezi vumilia mtu akimtukana.

Akiongea alipokuwa kwenye kipindi cha eNewz, Hussein Machozi alisema yeye lazima amtafute mtu yeyote ambaye anamtusi kwenye mitandao ya kijamii.

Staa huyo wa Bongofleva ameeleza kuwa yeye hawezi vumilia kama Ali Kiba na wasanii wengine ambao hawachukui hatua wanapotukanwa kwasababu yeye huumwa sana mtu akimtusi.

Tazama video hapo chini uone Hussein Machozi akieleza kwanini lazima yeye aadhibu yeyote anayemtusi kwenye mtendao wa kijamii:

Hussein Machozi achia wimbo mpya aliyotoa akiwa Italy

Hussein Machozi alirejea nchini Tanzania baada muda mrefu, staa huyo wa Bongofleva alisafiri kuenda Italy katika shughuli zake za masomo na muziki.

Soma pia: Hussein Machozi aelezea masaibu ambayo amekuwa akipitia nchini Italy

Hussein amerudi nyumbani akiwa na video yake mpya iliyoandaliwa Italy. Wimbo wake mpya unaitwa ‘Nipe Sikuachi’. Tazama video hapo chini:

https://www.youtube.com/watch?v=ZbK409Lt9P4&feature=youtu.be

Hussein Machozi aelezea masaibu ambayo amekuwa akipitia nchini Italy

Kwa muda mrefu staa wa bongo Hussein amwekuwa akiishi Italy lakini isa leo alirejea nchini kupumzika.

Alipata na wanahabari na wakazungumzia mambo mbali mbali ikiwemo mambo aliyoyakumba nchini humo. La kwanza ni chakula kwa sababu hoteli za huko hazina chakula kinachostahimili muislamu.

Sasa ilibidi akuwe akienda supermarket na kununua chakula alichokitaka.

Alieleza ya kwamba amesoma mengi kimuziki ambayo ata leta hapa nyumbani na kunufaisha sanaa.

Mtazame hapa kwenye hii video:

Hussein Machozi: Muziki wangu umeshika Kenya kuliko Tanzania

Hussein Machozi amerejea nchini Tanzania kutoka Italy, msanii huyo aliwasili jijini Dar es salaam usiku wa Jumatano.

Hussein alikua amesafiri kuenda Italy katika shughuli zake za masomo na muziki. Muimbaji huyo amerudi nyumbani akiwa na video yake mpya iliyoandaliwa Italy.

Akiongea na Bongo5, Hussein alisema kuwa hakuhamia Kenya kama wengi wadhaniavyo – muimbaji huyo amekaa Kenya sana na kufanya watu wengu kufikiri kuwa alihamia huko kabisa.

Hussein alisema kilichompeleka Kenya ni wimbo, alieleza kuwa anapata riziki kubwa Kenya kuliko Tanzania kwasababu muziki yake umeshika sana huko.

“Kenya nlikwenda kama nlivyokwenda Italy, jabo Italy ntarudi tena sababu sijamaliza kitu ambacho nlikua nafanya. Kenya nlikua nimeenda tu kwasababu kwanza huko ni nchi jarani alafu tena pia muziki wangu Kenya ulikua umeshika, umeshika hadi leo. Kwa hivyo riziki ulikua unapatika kule kubwa kuliko Tanzania…kwani nkajikuta mara nyingi naenda Kenya narudi Tanzania…Mbaka watu wengine walikua wanasema nimehama lakini hapana,”alisema Hussein Machozi.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.