Wasanii Wengi Hawaweki Maisha yao Halisi Katika Mitandao:-JB

Msanii wa bongo movies jacob steven amefunguk na kusema kuwa wasanii wengi wa bongo movies wako tofauti sana  na wale wa bongo fleva kwa sababu hawaweki uhaisia wa maisha yao na kazi yao katika mitandao yya kijamii kitu ambacho kiko tofauti sana.

JB anasema kuwa ukiangaia profile nyingi za bongo fleva artst utagundua tu kwa urahisi kuwa huyu ni msanii wa muziki lakini inakuwa ngumu sana kwa wale waigizaji kuweka profile yake hadharani kama wanavyofanya wengine.

akiongea na waandishi wa habari JB Anasema ‘wasanii wengi wa bongo movies hawawekagi maisha yao halis katika mitandao, tofauti sana na wale wa bongo fleva ambao wao  ukichungulia tu akaunti zao unakuwa unajua kuwa huyu ni msanii.hii yote ni kwa sababu ya watazania wengi ni malimbukeni wa matumizi ya mitandao ya kijamii.’

Ujumbe huu wa JB unawaendea moja kwa moja wasanii wanaotaka kuishi maisha  ambayo sio ya kwao, Jb anasema kuwa ni bora kuwa muwazi ili shabiki anapoamua kukukubali basi inakuwa amekubali kwa sababu ya vile ulivyo na sio tofauti.

Kutokuwa na Mtoto Hakujawahi Kunifanya Nikose Amani :-JB

Mkongwe wa nchini, Jacob Steven maarufu kama JB amewafungukia wale wote wanaodhani kuwa swala la kukosa mtoto kwenye ndoa linamfanya akose furaha maishani mwake.Wat wengi wamekuwa wakimshangaa msanii huyo kutoka na kuwa n afuraha na wala hakuwahi kulalamika kuhusu swala hilo.

Kwenye moja ya mahojioni aliyofanya Jb amefunguka na kusema “Ndio nakaribia miaka 50 na sina mtoto, sijabahatika kupata mtoto kwenye ndoa yangu, lakini kutokuwa na watoto maishani mwangu haijawahi kunifanya nikose amani au nimchukie mke wangu, Nampenda sana mke wangu na ipo siku naamini Mungu atatupatia mtoto au tusipopata kabisa pia tutamshukuru lakini sitaweza kukufuru.

Jb ameyasema hayo kukanusha imani ya baadhi ya watu wengi wanaoamini furaha ya ndoa ni mtoto na endapo atakosekana kwenye ndoa basi upendo kwa mwanaume utashuka kwa mkewe.

Wasanii Hawakumtumia Mzee Ipasavyo:-JB

Msanii wa bongo movie jacob steven amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi hawakumtumia Mzee Majuto ipasavyo kipenzi cha uzim wake hivyo hawakuachiwa urithi mwingi wa jinsi ya kufanya kazi kama alivyokuwa yeye mwenyewe.

Akiongea na waandishi alipokuwa katika viwanja vya Karimjee jijin Dar katika shughuli za kuaga mwili wa marehemu kabla haujasafirishwa kwenda tanga, JB anasema kuwa pamoja na kwamba hata yeye aliweza kucheza nae filamu mbili, ya shikamo baba na nakwenda kwa mwanangu lakini bado anaona kuwa bado kuna vitu vingi bado hawajajifunza kutoka kwao.

Jb anasema kuwa Mzee alikuwa mtu wa pekee na ndio maana hata kazi zake zimekuwa haaizchoshi machoni pa watu na zimekuwa zikipenda pamoja na kwamba zilikuwa za zamani na zimekaa katika soko kwa muda mrefu.

Mzee Majuto alitufundisha kuwa  tukithamini na kuheshimu kazi za filamu , tunaweza kuwa na mafanikio mengi kuliko tunavyofikiria. na tutaacha kulalamika kwa sababu vitu vingi anavyovimiliki vilikuwa vinatokana na sanaa yake.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.