Lady jay Dee Atoa Ufafanuzi Kuanguka kwa Wigi l

Msanii anaefanya vizuri sana katika muziki tangu miaka ya 90 mpaka sasa Lady Jay Dee aliamua kufunguka na kutoa ufafanuzi juu ya video iliyosambaa ikimuonyesha anacheza alipokuwa akifanya video ya wimbo wake mpya wa anaweza ambapo mwanadada huyo alikatiza kucheza kutokana na wigi alilokuwa amevaa kichwani kuangauka,

Wadada wengi wamekuwa wakivaa mawigi ili kuficha nywele zao kichwani na wengine kupata aibu sehemu za watu hasa pale ambapo wigi linlaegea na kushindwa kukaa kichwani.

Akiongea na bongo 5 huku akicheka , lady jay dee alisema kuwa hiyo ni ajali kazini”lilianguka..ilikuwa kwamba wigi lilianguka chini na ikawa ni kama ajali kazini“-huku akicheka Jay Dee aliongea.

Huku akifafanua kama kuna uwepo wa project nyingine baada ya hii ya anaweza. Jay Dee anasema kuwa ni mapema sana kwa sasa kuzungumzia swala hilo kwa sababu hata hii iliyopo sasa bado ndio kwanza imepokelewa hivyo anawaacha mashabiki kufurahia swala hilo kwa sasa.

Lady Jay Dee afichua kinachomfanya ku-hit kwa miaka 17 sasa

Jay Dee amesisitiza kuwa mafanikio yake kwenye muziki ulipigwa jeki na hatua aliochukua miaka kumi na saba iliopita.

Mwanamziki huyo anasema kuwa kitendo cha yeye kutolewa na sifa ndiyo kimemfanya kuendelea ku-hit katika sanaa ya muziki.

Jay alisema wasanii wengi hupotea baada ya kuwa staa na kushindwa kutoa nyimbo zingine kwa sababu ya kulewa na sifa.

Msanii huyo alifichua kwamba kutolewa na sifa ndiyo siri pekee iliyomfanya aweze kupita katika vipindi vyote vigumu maishani mwake.

“Ukifanya ngoma na watu wakakujua utakuwa staa lakini usilewe sifa ukilewa mapema utalala alafu utashindwa kuamka…ni miaka kumi na saba sasa, sijawahi kulewa na kila siku naona kama nahitaji kujifunza kitu kipya” Alisema Jay Dee.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.