“Nitamlea Mwanangu Katika Misingi Ya Dini”-Jike Shupa

Video Queen aliyejizolea umaarufu Baada ya kuonekana kwenye video ya wimbo wa Nuh Mziwanda ‘Jike Shupa’ Zena Abdullah maarufu kama Jike Shupa amefunguka kuhusu ujauzito Wake.

Jike Shupa amesema kuwa akiwa katika miezi michache kukaribia kujifungua mtoto wake ameweka wazi kuwa anampango wa kumlea Mtoto Wake katika misingi ya kidini.

Wakati mwingine mipango kabla ya tukio ‘inamata’, maana Jike Shupa amejiapiza hivyo miezi minne kabla ya kujifungua kwake, ambapo amesema, akizubaa katika malezi mwanaye ajaye anaweza kufuata mkumbo wa maisha mabaya.

Natarajia kujifungua mwezi wa nne Mungu akipenda, sijaenda kupima ili nijue nitajifungua mtoto wa jinsia gani, lakini natarajia siku za hivi karibuni nifanye hivyo kwa kuwa natamani nijue nimebeba kiumbe cha jinsia gani“.

 

Jike Shupa Adai Ujauzito Ndio Umemfanya Awe Kimya

Video vixen na muandaaji maarufu wa vibao kata Zena Abdallah maarufu kama Jike Shupa amefungukia ukimya wake  na kuweka wazi kinachomfanya awe kimya ni ujauzito alionao.

Jike Shupa amesema amekuwa kimya sana kwenye mitandao ya kijamii kutokana na majukumu ya kubeba ujauzito lakini amesema akishajifungua tu mtoto wake atarudi kama  kawaida.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Jike Shupa alisema kuwa, watu hawasikii purupukushani zake ila akishajifungua, kila mtu atajua ameibuka tena mjini.

Najua mjini kumepoa sana kwa sababu mimi kubwa lao sisikiki, lakini ngoja nizae kwanza, nikikaa sawa, wataisoma namba na vimbwanga vyangu kama kawa“.

 

Jike Shupa: Baada ya Kutoa Mimba Nyingi Sasa Nimeamua Kuzaa

Msanii Bongo Movie na video queen wa Bongo fleva Zena Abdallah ‘Jike shupa’ aliyejizolea umaarufu baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa Nuh Mziwanda Jike Shupa.

Global Publishers, wanatipoti kuwa siku za nyuma Jike Shupa alishawahi Kula kiapo kuwa kamwe hatozaa na mwanaume mwingine zaidi ya mtoto aliyezaa na msanii mkongwe wa Bongo fleva Juma Kassimu Nature.

Jike Shupa amevunja kiapo hiko baada ya kuonekana akiwa na kitumbo na ujauzito wake mwingine.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, baada ya Jike shupa kuhojiwa juu ya imekuwaje kuamua kuvunja kiapo alichoweka ambapo alikiri kuwa alishatoa mimba nyingi hivyo kwa sasa ameamua kumzalia mpenzi wake aliyemtaja kwa jina moja la Montelego kwani anahitaji mtoto.

Siku hizi nashindwa kujichanganya kama zamani kwa sababu ya ujauzito na nimeamua kuvunja kiapo na kubeba mimba kwa sababu ninampenda sana mpenzi wangu na ni muda mrefu anahitaji mtoto, nami nimeona nimridhishe nafsi yake“.

Waliotembea na Mimi Wakapime UKIMWI ;-Jike shupa

Mwanadada  zena abdala maadufu kama jike shupa amefunguka na kuwapa pole wale wote aliahikutoka nao kimapenzi na kuwashauri wakapime ukimwi .maneno hayo ya jike shupa yanakuja baada ya mwanadada huyo kuweka picha katika ukurasa wake wa instagrama ambazo zilizua mjadala kutokana na mapaja yake kuonekana kuwa na vipele vingi.

Katika kumsema sana katika mtandao wa instagram baadhi ya watu walianza kumsema na kumwambia kuwa ukiachana na kosa kuweka picha kazma hizo katika mtandao wa instagram lakini pia mapaja yake wala hayana hadhi ya kuwekwa katika mtandao  kutokana na jinsi yalivyo.

Hata hivyo baada ya kusemwa sana , Jike shupa aliamua kuwa jibu na kusema kuwa kama kuna mtu yoyote aliwahi kutembea nae basi aende akapime ukimwi .

sasa watu wameona kuwa hilo ndo la maana sana , hiyo picha ni treta tu lakini ujumbe wenyewe ni kuwa kama kuna mtu aliwahi kutembea na mimi akapime maambukizi ya virusi vya UKIMWI.

Jike Shupa Avunjiwa Mlango Kisa Mashoga

Mwanadada aliyepata umaarufu sana baada ya utokea katika wimbo wa Jike shupa wa Nuh Mziwanda ambae kwa mud amekuwa akikumbwa na skendo ya kutunza mashoga na baadae kutunza watumiaji wa unga amekutwa na kisanga kipya  bada ya watu kuja nyumbani kwake na kumvunjia mlango.Mwanadada huyo alivunjiwa mlango na ndugu zake kwa madai kuwa hawataki ndugu yao akae na wanaume tata (mashoga) ambao amekuwa akikaa nao kwa siku nyingi sasa.

Ndugu wa karibu wa mwanadada huyo wamesema kuwa kwa muda mrefu ndugu ao amekuwa akiishi na watu hao na kufanya hata ndugu zake kushindwa kumtembelea nyumbani kwake.

Unajua watu wengi ambao ni ndugu wa jike shupa wamekuwa wakigoma kuja kwa jike shupa kwa sababu ya hao watu wake,karibia watu wake wote wa karibu na jike shupa ni wanaume tata.

Aliyekwa anatoa habari hiyo alisema kuwa ndugu zake walijipanga na kufika nyumbani kwa jike shupa majira ya saa moja usiku na kugonga mlango ambapo baada ya kugonga jike shupa aliwaona kwa kuwachungulia dirishani kisha akanyamaza kimya hakufungua.

Baada ya kugoma kufungua mlango huku wakiwa na uhakika kuwa yupo ndani ndipo walipopatwa na jazba sana kwa sababu ndugu zake ni washika dini sana.Kilichofuata ni kuusukuma mlango kwa nguvu mpaka waliovunja , hawakuamini macho yao.

Alipotafutwa Jike Shupa kuelezea tuio ilo alisikiaka akisema kwa tukio ilo lilishaisha siku nyingi sana na hata waliokuwa wamefanya hivyo walikuwa ndugu zangu.

Mbona iyo ishu ilishaisha , ilikuwa ni kwa sababu ya hawa ndugu zet( mashoga), wanasema kuwa hawapendi nikae nao, lakini mimi naona ni kama watu wengine tu.

 

 

Jike Shupa Apata Tetesi za Kufuga Mateja Nyumbani Kwake.

Mwanadada anayeuza sura katika video za wasanii mbalimbali almaarufu  kama JikeShupa amekumbwa na tetesi za kufuga watumiaji wa madawa ya kulevya nyumbani kwake na kwamba mateja hao wamekuwa na athari kubwa katika mtaa huo.

Hivi karibuni mwanadada huyo alifunguka na kukubali kuwa alikuwa akikaa na mdogo wake na mbunge wa chadema Esther Bulaya ambae mdogo wake ameathirika na matumizi ya madawa ya kulevya ambae alikuwa akihitaji mtu wa karibu wa kukaa nae kwa kipindi hiki ambacho alikuwa akipatiwa matibabu.

Jike shupa ambae anakaa maeneo ya Mwananyamala hospitali inasemekana kuwa amekuwa akikaa na watumiaji wa madawa ya kulevya zaidi ya mmoja na kwamba amekuwa akiishi nao kinyume cha utaratibu kitu kinachowatia wasiwasi hata majirani zake.

Jike shupa anawafuga mateja kwakweli kwa sababu anachumba maarumu kabisa ambacho wanakaa,na wengi wao ni wale wanaotumia madawa kwa ajili ya kuacha unga.watu wanadai kuwa kuna kitu atakuwa anafaidi kwa sababu anakaa nao na kuna muda watu wanalaamika kuwa wanapora alafu wanamletea yeye mama yao.-Aliongea mmoja wa wakazi wa mtaa anaokaa jike shupa

Alipotafutwa jike shupa kujibu tuhuma hizo alikubali kuwa ni kweli amekuwa akikaa na watu hao kwa muda mrefu kwa sababu walikuwa wakituma dawa za kuacha madawa ya kulevya lakini sasa hivi walisharudi makwao na wala hawapori watu.

sio kweli kwamba walikuwa wanapora watu mitaani,lakini walishamaliza dawa za kufanya waache  kutumia unga na sasa waisharudi makwao.-Alifunguka jike shupa.

Hpo awali jike shupa alishawahi kukumbwa na tetesi za kuwa anawafuga mashoga nyumbani kwake na kufikia hatua ya kugombana na majirani zake.

Jike Shupa Akumbwa na Skendo ya Kufuga Mateja Nyumbani Kwake

Video queen maarufu Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ amekumbwa na skendo nyingine ambapo amedaiwa kufuga mateja wa unga au watu wanaotumia madawa ya kulevya nyumbani kwake.

Jike Shupa alijipatia umaarufu kwa mara ya kwanza baada ya kutokea kwenye video ya wimbo wa jike shupa ulioimbwa na Nuh Mziwanda ambao uliodhamiria kumponda mpenzi wake wa zamani Shilole.

Hivi karibuni Jike Shupa alikiri kuwa anaishi na mdogo wa Mbunge wa Bunda mjini Esther Bulaya, Deus Bulaya aliyeathirika na matumizi ya madawa ya kulevya ambapo anaishi naye nyumbani kwake maeneo ya Mwananyamala hospitali.

Lakini habari zilizolifikia gazeti la Ijumaa Wikienda kutoka kwa moja ya majirani wa jike Shupa anayeitwa Hassan zimedai kuwa amekuwa akiwafuga vijana hao kwa wingi bila utaratibu wowote nyumbani kwake:

Jike Shupa anawafuga mateja wengi sana kwa maana ana chumba maalumu kwa ajili yao na wengi ni wale wanaotumia dawa kwa ajili ya kuacha unga (methadone) watu wanadai kuna vitu anafaidika nao kwani watu kama hao kuna vitu wanapora na kumletea yeye kama mama yao”.

Alipotafutwa na Motomoto News na kuulizwa kuhusu tuhuma hizo Jike shupa alikiri kuwa ni kweli alikuwa anawasaidia vijana waliokuwa wanatumia methadone lakini kwa sasa wamesharudi kwao.

Jike shupa alishatuhumiwa kuwa alikuwa anafuga vijana ambao walikuwa wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (Mashoga) siku za nyuma nyumbani kwake hapo hapo.

Jike Shupa Ageukia Kwenye Umama Ntilie

Mwanadadad ambae amekuwa akiuza nyago kwenye video mbalimbali  Jike shupa ameamua kufanya kazi nyingine ambayo itakuwa ikimuingizia kipato zaidi kuliko kukaa na kubweteka katika sekta moja kwa sababu hajui kazi hiyo itamfikisha wapi.Mwanadada huyo amesema kuwa ameona sasa hivi vyuma vimekaza katika sanaa anayoifanya kwaiyo ni bora ageuka na upande mwingine kutafuta maisha.

Jike Shupa amesema kuwa kwa sasa maisha yamekuwa magumu na ameona aache kuzubaa na kufanya starehe na wanaume mashoga na kuingia katika kutafuta kazi ya kufanya kwa sababu mambo yanazidi kuwa tata.

Yaan niliona ntakufa njaa kwaio nimeona ni bora kuwafukuza wale mashoga kwangu, na kuanza kufanya kazi  za kupika kwenye shughuli mbalimbali kwaio ninachukua tenda sehemu mbalimbali na kupika na watu wangu, naona hii inalipa kwa sababu tangu nimeamua kuacha hizo starehe  na ninapata ela kwa kupitia nguvu zangu mwenyewe.

Mwanadada huyo amekiri kuwa alikuwa na tabia ya kuwafuga wanaume mashoga nyumbani kwake na kufanya starehe huku wakitegemea kutumia ela za kudanga kutoja kwa wanaume lakini sasa hivi ameona ni bora abadilike.

Jike Shupa arudi CCM kumfuata Wema

Mwanadada aliepata umarufu mkubwa baada ya kutokea katika video ya msanii Nuh Mziwanda iliyojulikana kama Jike Shupa na kulivaa jina ilo kuwa ndio jina lake maarufu ametanga pia kurudi CCM baada ya mwandada anaempenda kurudi ccm akitokea chadema.

Wema Sepetu alitangaa kurudi CCM,Wikiendi iliyopita akitokea Chadema ambapo alikuwa amehamia mwanzani mwa mwaka huu akiwa na mama yake,

Jike Shupa ambae pia alihamia Chadema siku za nyuma baada ya Wema kuhamia huko alisema kuwa kwa sababu ana mpenda Wema atamfata kokote anakoenda ilimradi kuwa anampenda sana mwanadada huyo.Hivyo ndio maana hata wema alipotangaza kurudi ccm tena mwanadada jike shupa akusita kwenda nae Wema Sepetu.

Akiwa ni moja ya wanadada wenye ushawishi mkubwa nchini Tanzania kupitia mitandao ya kijamii  hivyo watu wengi wataendana na mwitikio huo wa kuhama chama kutokana na kumpenda mwanadada huyo.

Kisa Picha Za Utupu, Jike Shupa Atupiwa Vitu Nje

Mwanadada  Zena Abdalah maarufu kama Jike shupa ambae alipata umaarufu sana baada ya kutokea katika video ya msanii Nuh Mziwanda iliyojulikana kama jike shupa ambapo yeye alitokea na kufananishwa na Shiloleh kwa jinsi alivyoweza kuwasilisha maisha ya msanii huyo na aliyekuwa mpenzi wake shilole.

Wiki iliyopita mwandada huyo aliingia matatani baada ya kufukuzwa katika nyumba anayokaa ya kupanga baada ya kushutumiwa kurushwa picha za uchi katika mtandao wa instagram na kuwakwaza watu anaokaa nao katika nyumba hiyo.

Jike shupa alikumbwa na aibu hiyo usiku wa maneno baada ya mwenye nyumba kumfukuza  huku sababu ikiwa ni mwanadada huyo kutupia picha za utupu katika mtandao wa instagram, hivyo kuwakwaza watoto wa  baba mwenye nyumba ambae inasemekana kuwa ni mshika dini sana.

Hata hivyo chanzo cha habari kInasemakuwa mwanadada huyo amekuwa na tabia hiyo ya kuweka picha za utupu katika mitandao kwa mara nyingi sana kiasi kwamba wapangaji wenzake wamekuwa wakikwazika sana, na kusema kuwa hiyo ni kinyume na maadili kabisa kwa mwanamke kama yeye ambae tayari ameshafikia utu uzima.

Mpangaji mmoja wa nyumba hiyo anasema kuwa katika nyumba hiyo  wapangaji wote wameshika dini hivyo juzi kati jike shupa alivyoweka picha katika mtandao wanawake wakicheza uchi iliwakera sana watoto wa mwenye nyumba anayokaa na kumwambia atafute nyumba nyingine.

Hata hivyo inasemekana kuwa watoto wa mwenye nyumba hiyo walishamuonya jike shupa zaidi ya mara moja lakini hakuwa anasikia na aliendelea na tabia yake iyo, hivyo walimwambia atafute nyumba nyingine lakini kitu cha kushangaza ni kwamba mwanadada huyo aliwabishia na kuanza kuwajia juu watoto hao ndio walipopandwa na hasira na kumtolea vitu nje kwa mkurushia.

Hata hivyo baada ya jike shupa kutafutwa ili kuthibitshahayo alisema kuwa

yaani wale watu wamenizingua sana,mtu nimepangisha kwa fedha zangu mwenyewe,kwaio mimi nisitangaze  shoo yangu, sasa ntakula wapi na ntapata wapi ela ya kodi, hata hivyo haijaniumiza nishapata nyumba nyingine.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.