Mke Wangu Hakunilazimisha Kumuoa. :-Joti

Msanii wa maigizo ya vichekesho nchini Joti amefunguka na kukanushataarifa kuwa mke wake ndio ilikuwa sababu ya yeye kuoa kwa sababu alikuwa akimlazimisha kila siku kutaka kufunga ndoa, Joti anasema kuwa alipoona muda muafaka wa yeye kuoa umefika ndipo alipoamua kufunga ndao.

Hata hivyo Joti anasema kuwa pamoja na kwamba walikuwa katika mahasiano , mke wake mara nyingi alikuwa akimkumbusha kuhusu swala la ndoa lakini yeye alikuwa akifanya kama ahasiki amaneno anayoambiwa na mke wake mpaka pale alipoona kuwa sasa mke wake amenyamaza na muda umefika ndipo alipoamua kufunga ndoa.

Akiongea kwenye Leo Tena ya Clouds media Joti anasema “”wakatai tupo kwenye mahusiano mke wake alikuwa ananikumbusha sana kumuoa,kila akiniambia nilikuwa namwambia tulia, mpaka alipoacha kunkumbusha ndipo nilipomua bila kulazimisha

Joti Atoa Ufafanuzi Kuhusu Kubomolewa kwa Nyumba Yake.

Asubui kulikuwa na habari pich zikisambaa kuhusu nyumba yaa msanii Joti kuwekwa alama ya x ikimaanisha kubomoa na pia ikasemekana kuwa nyumba hiyo imejnegwa katika eneo la barabara hivyo inabidi kubomolewa, lakini msanii huyo ameona kuwatoa wasawasi mashabiki wake na kuwaambia taarifa rasmi kuhusu swala hilo.

Akiongea na Clouds fm, msanii Joti anasema kuwa ni kweli eneo wanalikaa kuna upanuzi wa barabara lakini swala hilo halitaathiri nyumba nzima bali watatakiwa kubomoa ukuta tu.

wanapanua barabara huku kwetu lakini upanuzi wa barabara hautahuisha kubomolewa kwa nyumba bali ni ukuta tu, wengi wamejua kuwa ni nyumba lakini sio nyumba ni ukuta tu.Aliongea joti.

Kwa mujiwa wa Afisa Manispaa huko kigamboni anasema kuwa katika eneo hili nyumba kama 100 ziliwekwa alama kwa ajili ya kupisha upanuzi wa barabara wa eneo hilo.

Nyumba ya Joti Kubomolewa

Habari zilizosambaa leo asubuhi katika mitandao ya kijamii na katika magazeti ni kuhusu nyumba kubwa ya msanii wa vichekesho na msanii anaetumika katika matangazo mengi ya kijamjii hasa kutokna na ukubwa wa kazi zak na umbo lake linalomfanya kuwa na uhuru wa kufanya kitu chochote .

Nyumba hiyo ambayo bado ni mpya , inasmekana kubomolewa huku oicha zikiwa zimesambaa msanii huyo akiwa  na baadhi ya maafisa wa polisi akiwa anazungumza nao huku nyumba hiyo ikionekana kuwa na michoro ya x ikibaanisha kubomolewa.

hHata hivyo, wadau na watu mbalimbaliwameshauri kuwa pale watu wanapotaka kununua kiwanja au nyumba ni bora kuuliza kwa undani eneo hilo unalonunua linakuwa na matumizi gani ya kijamii isije kuwa kama haya yaliyomkuta joto kuwa hakuwa anaua kama ni eneo la barabara.

Mashabiki Wahoji Kiduku Cha Joti Kanisani

Ikiwa bado ndoa mbichi   na vyombo vya habari vikiwa vimechachamaa kusambaza picha za matukio ya harusi ya mchekeshaji mkongwe na balozi wa makampuni mengi nchini Joti, baadhi ya mashabiki na vyombo vya habari vimehoji muonekana wa bwana harusi tena hasa alipokuwa maeneo ya kanisani katika ndoa hiyo.

Joti ambae anamuonekana wa nywele za kiduku cha aina yake amefunga ndoa jumamosi iliyopita na mkewe huyu na sherehe kufanyikia akatika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salaam.

staili ya nywele ya msanii huyo ambayo ni kiduku imekuwa ikiaminika kuwa ni fashion ya kihuni na sehemu za heshima haipaswi kuwepo hasa kanisani.sasa je joti ameruhusiwaje kufunga ndoa na style hiyo ikiwa ni staili ya kihuni na haikubaliki kimaadili.

Wakiwa kanisani , mmoja wa wahumini alisikika akinongona na mwandishi wa gazeti moja pendwa nchini”sasa hiki ndo kitu gani jamani, yanai kweli padri anaruhusu ili jambo lifanyikie kanisani kweli?

‘Huu mtindo wa nywele si mtindo wa viajana wa kihuni, wanaonyesha huko mtaani,wanaruhusuje hili jambo kanisani, au kwa sababu  huyo ni kijana maarufu’ mwanamke mmoja alisikika akisema pia.

Inawezekana ikawa ni kitu kidogo kwa baadhi ya mashabiki lakini, jotiambae ni balozi wa makampuni mengi nchi, muonekano wake ni biashara yake,hivyo yeye kubadilisha stle ya kunyoa kwa tukio la siki moja ilhali bado ana maeneo mengi ya kutumia muonekano huo ni vigumu .

Harusi ya msanii huyo ilifana sana baada ya joti kufunga ndoa na mkewe alikuwa mpenzi wake wa siku nyingi, waliohudhuria katika harusi hiyo walikuwa wengi akiwepo Mpoki na wasanii wote waliokuwa wakiunda kundi la ze comedy,Wolper, Steve Nyerere, Mboni Masimba na wengine wengi.

Muonekano wa Joti na mkewe wakiwa kanisani na ukumbini, Joti akiwa na kiduku. 

Matukio Katika Picha: Ndoa Ya Mchekeshaji Joti

Msanii na mchekeshaji  mkongwe na maarufu alieanza kazi za uuchekeshaji kwa muda mrefu joti amefunga ndoa jumamosi iliyopita. Ndoa yake ni moja kati ya ndoa zinazoingia katika orodha ya ndoa zilizofana sana Tanzania.Ndoa hiyo ambayo ilfanyikia Mlimani City jijini Dar Es Salam na kuhudhuriwa na watu mashuhuri  ilikuwa ya aina yake.Hizi ni baadhi ya picha za ndoa hiyo

Joti akiwa na mpambe wake Sekion david

joti akiwa na mke wake

joti akifurahi jambo na mkewe , kulia ni wanandoa na familia.

Joti na mkewe wakiwa na furaha.

Baadhi ya watu waliodhuria ukumbini kusherekea pamoja nae

 

 

Harusi Ya Mchekeshaji Joti Imeiva

Msanii wa maigizo na mchekeshaji maarufu tanzania Joti, anatarajia kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu hivi karibuni.msanii huyo ambae amekuwa akionekana katika matangazo ya bidhaa tofuati tofauti tanzania ameonekana  hivi karibuni katika mitandao ya kijamii yeye na mpenzi wake huyo katika picha za pamoja ikiwa ni pre-wedding photshop.

Joti ambae alianza maigizo ya uchekeshaji miaka mingi nyuma na baadae kuingia katika kundi la ze comedy waliokuwa wakirusha matangazo yao katika Televisheni ya Taifa anategemea kufunga ndoa na sherehe kufanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar Es Salam.

Akiandika katika moja ya post zake katika ukurasa wake wa instahram Joti aLiweka picha aliokuwa pamoja na mkewe huyo na kuandika “alilopanga mungu..” hata hivyo baadhi ya picha zilimuonyesha msanii huyo akiwa na rafiki zake wa karibu katika send-off party ya mke wake.

Baadhi ya mashabiki wameonekana kufurahishwa na jambo hilo na kumpongeza msanii huyo, huku wengine wakidhania ni utani kama ilivyozoeleka hapa awali ambapo Joti amekuwa akiweka picha za harusi na wadada tofauti  kumbe alikuwa katika moja ya kazi zake za matangazo.

Baadhi ya wasanii wenzie walimpongeza msanii huyo na mmoja wapo alikuwa ni mchekeshaji mwenzie  Masanja Mkandamizaji aliyempongeza kwa kuacha chama la makapela.

Moja ya picha zilizopo mtandaoni zikimuonesha joti akiwa na Sekion David katika send-off part ya mkewe

Joti akiwa na mkewe mtarajiwa katika picha ya pamoja katika send off party ya mkewe.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.