Ndoa Ya Juma Kapuya na Binti Wa Miaka 25 Yazua Gumzo

Ndoa ya aliyewahi kuwa Mbunge wa Urambo mkoani Tabora, miaka ya nyuma Juma Kapuya mwenye umri wa miaka 74  na binti wa miaka 25 ambayo ilifungwa siku ya jumapili imezua gumzo kubwa katika Mitandao ya kijamii.

Picha na video kadhaa zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii zimemuonyesha Profesa Juma Kapuya ambaye ni mtu mzima kupitiliza akimuoa binti huyo mdogo ambaye anaweza akawa binti yake aliyeatambulika kama Mwajuma Mwiniko na ndoa ilifungwa wilayani Urambo, mkoani Tabora.

Profesa Juma Kapuya alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kuanzia mwaka 1997 hadi 2005 na baadaye akateuliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Ulinzi (mwaka 2006) na kisha kuwa Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo nafasi aliyoteuliwa mwaka 2008.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.