Tuliokulia Uswahilini Ndio Tunafanikiwa Kimaisha :-Kidoa

Mwanadada Asha Salum maarufu kama Kidoa amabe amepata zaidi umaarufu kutoka katika tamthilia ya Huba amefunguka na kujisifia na kuringa huku akisema kuwa anaona fahari sana kwa maisha yake ya kukulia uswahilini kwa sababu anaona mafanikio yake kwa sasa.

Kidoa anasema kuwa kuna watu wengi amekuwa akiwaona wakikulia maisha ya uswahilini ambao kwa sasa hivi wanafanya vizuri kimaisha na hata ukiwalinganisha na wale waliokulia maisha safi kuna kuwa na utofauti mkubwa.

Kidoa anasema kuwa hatokaa kamwe hajute kukulia uswahili kwa sababu maisha ya huko yanawafanya kila siku kufikiria kitu kipya katika maisha.

unajua kuwa ukiwaona wasichana wengi wamefanikiwa unaweza usiamini kama wametokea uswahilini, tena kwenye maisha ya tau sana lakini ndio wanakuwa kioo cha jamii.kwa mfano kama leo uweiz kuamini kuwa mimi nimetokea uswahilini kweny kila kituko lakini leo hii ninaweza kusimama mbele za watu na nikaongea kitu na kusikilizwa.

Kidoa Arudi Kwenye Tabia Yake Ya Ufuksa

Mwanadada  wa filamu za bongo Asha Salum  Maarufu kama Kidoa amedaiwa kurudia tabia yake ya kupiga picha za uchi na kuzirusha mitandaoni baada ya kusimama kwa muda mrefu .Kidoa ambae kipindi cha nyuma aliacha tabia hiyo kutokana na kuwa na mahusiano na mwanaume aliyesemakana kuwa ni kigogo ambae alimkataza kufanya tabia hiyo ya kupiga picha za uchi wala kuvaa nguo za kuonyesha nguo zake.

Kidoa ambae alikuwa na tabia hiyo tangu zamani alisimama tabia hiyo kutokana na pedeshe huyo kumkataza kufanya vitu hivyo kwa kuwa alikuwa akimuhudumia hivyo alikuwa chini ya himaya yake hivyo alikuwa anapaswa kufanya kile anachoambiwa na pedeshee huyo.

Hata hivyo , baada ya kumtafuta Kidoa GPL, walifanikiwa kumpata na kumuuliza tetesi hizo ambapo mwanadada huyo alisema kuwa watu wamekuwa wakimsema bila kujua maisha yake yakoje, hata hivyo mwanadada huyo alisema kuwa watu wanasema nimeachwa kwa sababu tu kuweka picha ambayo ilikuwa ikimuonyesha maungo yake akiwa amevaa  nguo za kuogelea,akiendelea kujitetea anasema kuwa hizo ni nguo ambazo alikuwa akizipenda tangu zamani lakini sio kwamba ameacha.

Watu wanapenda sana kufatilia maisha yangu , najua hayo yote yameibuka kwa sababu nimeweka picha nikiwa na nguo  za ndani  tu.mavazi hayo nilikuwa nayapenda sana huko siku za nyuma lakini sio kweli kuwa mwanaume niliyekuwa nae ameniacha, niliweka picha hizo kujipumzisha tu. -Aliongea Kidoa alipotafutwa kwa simu

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.