Ben Pol Atangaza Kolabo Yake na Kiss Daniel Wa Nigeria

Mwanamuziki wa Bongo fleva Ben Pol anayetamba kwa muziki wake wa miondoko ya RnB amefungukia mipango yake ya kufanya kazi na wasanii wa kimataifa zaidi.

Ben Pol ameweka wazi kuwa  Kolabo yake ya kwanza itakuwa na staa kutoka Nigeria Kiss Daniel ambaye itatoka hivi karibuni na it aende kwa jina la Zai.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Showbiz Xtra, Ben Pol alisema kwamba mwaka huu amejipanga kwa makubwa na kolabo yake hiyo ni mwanzo wa hayo makubwa ambayo anatarajia kuyatoa kwani anazaidi ya kolabo tatu za kimataifa mwaka huu ambazo zitampeleka ‘level’ nyingine.

Mwaka huu ninatarajia kutoka na kazi zaidi ya tatu za kimataifa na ujio wangu na Kiss Daniel ni mwanzo wa kazi hizo, mashabiki wangu wakae mkao wa kula”.

Lakini pia Ben Pol ametangaza ujio wa wimbo huo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ben Pol ameachia ngoma yake na Ebitoke inayokwenda kwa jina la natuliza boli ambayo inafanya vizuri bado.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.