Maimartha Kuamisha Majeshi kwa Mobeto, Amkimbia Zari.

Mwanadada Maiamartha wa Jesse ambae amejipatia umaaarufu sana kwa kupitia kazi yake ya utangazaji na sasa hivi ni MC amejikuta akihamisha majeshi na mapenzi aliyokuwa nayo kwa mwanamama Zari kutoka Uganda na kuanza kumpenda na kumpalilia Hamisa mobeto kutoka Tanzania .

Kwa hali isiyo ya kawaida mwanadada Maimartha alikuwa akimsifia sana Zari hapo awali  na alishawahi mpaka kumwambai hamisa kuwa ajiengue katika kuweka bifu na Zari kwa sababu Zari sio saizi yake na wala hana haja ya kuwa akigombana nae sana katika mitandao kwa sababu ya mwanaume.

Hata hivyo , Maimartha alianza kuonekana akihama upande huo taratibu na hata kufikia hatua ya kusema kuwa Zari ana roho mbaya baada ya  kusikika kuwa Zari alikataa kuwakaribisha nyumbani kwao kwa ajili ya sherehe ya mtoto wao.

Baada ya Hamisa kutoa wimbo wake hivi karibuni, Maimartha kupitia katika ukurasa wake aliweka post ya kumpongeza hamisa kwa kuandika “Hamisa…Go girl i feel hot..” baada ya Hamisa kutoa wimbo wake wa madam Hero.

Sitokei Katika Wimbo Kama Hauzidi Salome:-Mobeto

Mwanadada ambae ni video Queen wa muda mrefu lakini kwa sasa amejiingiza katika biashara ya nguo na ujasiriamali kwa ujumla amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hana mpango wa kutokea tena katika video za wasaii mbalimbali kama alivyokuwa akifanya mwanzoni lakii atatokea katika wimbo ambao utakuwa umezidi uzuri kuliko ule wa salome ambao ndio ulikwa wimbo wake wa mwisho.

Hamisa Mobeto ambae wimbo wake wa mwisho kutokea ulikuwa ule wa salome alioimba msanii Diamond ambae ni mzazi mweznie kwa sasa, anasema kuwa ili msanii mwingine atake yeye kutokea katika video yake ni lazima wimbo uwe mzuri kuliko ule aliofanya mwsiho ambao ndio salome.

sifanyi video tum ninafanya na nimefanya nyingi lakini nachagua wimbo, ninachagua maudhui , ninachagua kila kitu so for me  kutokea kwenye wimbo tena  inabidi uwe mzuri kuzidi ule  wa salome.

Maimartha Ang’ang’ana Na Hamisa Mobeto.

Mwanadada ambae ni moja ya  watangazaji maarufu nchini Maimartha wa Jesse ameibukana kusema hata kama Hamisa Mobeto amekaa kusikiliza ushauri wake hatokaa aache kumfunda kwa sababu yeye anamuonea huruma kwa sababu badala ya kutenga muda kwa ajili ya familia yake na kufanya mambo yake ya maendeleo amekuwa akifanya vitu ambavyo vinamfanya kushindana na Zari katika mitandao ilhali mwanamke anaeshindana nae anamzidi kwa kila kitu.

Mara ya kwanza Maimartha aliandika katika ukurasa wake wa instagram na kumshauri Hamisa kuacha kurumbana na Zari kwa sababu kwanza anakuwa anamuumiza mama yake kwa kuwa anatukana matusi na Team Zari lakini pia angeachana na kukubali matokea kuwa Diamond hawezi kumuoa kwaio ampende na kupatana na Zari ili aweze kulea mtoto wake vizuri.

Lakini kitu cha ajabu ni kwamba hamisa hakutaka kuupokea ujumbe huo  kama ambavyo maimartha alihisi angeweza kuupokea zaidi ya kumwambia kuwa ushauru huo angeufanyia kazi kwa familia yake.

Mairmatha alisema kuwa pamoja na majibu mabaya ya Hamisa lakini bado yeye hatoaacha kumshauri  kwa sababu anaona kabisa kuwa anapotea.  Lakini pia anaamini kuwa hata kama anamjibu vibaya lakini meseji anazompa anazisoma na anajifunza kitu hata kama hataki kuonyesha kuwa anajali.

Kiukweli niliamua kumshauri na nitaendelea kumshauri ingawa yeyey alinijibu vibaya, ila ninachoamini ni kwamba ujumbe unamfikia na anatakiwa kujirekebisha tu  na ni kweli lile tamasha halikuwa ya hadhi yake.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.