Najuta Kupoteza Miaka 6 Kwa Ajili ya Makomandoo-Muki

Baada ya habari kusambaa kuwa kundi la muziki  la Makomandoo limesambaratika  habari amabzo ziliwekwa wazi  na Fredy Whine ambae ni mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, na  kusema kuwa kwa sasa kundi hilo limekufa kwa sababu mwenzake Muki yuko busy na familia na kwamba  familia yake inambana sana kufikia hatu akushindwa kufanya kazi.

Lakini baada ya taarifa hizo kusambaa , Muki pia ameamua kufunguka na kusema kuwa sio kweli kuwa familia imemfanya yeye na Fredy waachana na washindwe kufanya kazi za muziki.Hata hivyo Muki amesema kuwa alishangaa sana kuona habari kama hizo kwenye vyombo vya habari na hata ndugu zake walitaka kujua kama wamegombana.

 Alitaka kunipeleka polisi kisa gari,tukafanya nyimbo lakini nikawa nasikia anafuta sauti zangu,Nilimwambia kuwa nimeshachoka na isiwe shida itafika sehemu mimi nitaamua maamuzi magumu lakini kabla ya mimi kuamua nashukuru kaanza kuamua mwenzangu.

Ilo ni tatizo lingine ambalo ananitangazia kuhusu familia, kwamba inafanya  nisifanye muziki  lakini hata yeye ana familia pia na familia yake haijali kabisa, na ndio maana anaona mimi nimebanwa na familia , hakuna ukweli huo.

Baada ya kuongea hayo yote , Muki alisema kuwa sababu kubwa ya wao kugombana ni kwa sababu  msanii mwenzake huyo ana roho mbaya hivyo hawawezi kukaa wote na kufanya kazi.

Tatizo kubwa la ndugu yangu yule ana roho mbaya,mpaka mimi mwenyewe uwa namwambiaga kuwa wewe sidhani kama kwa roho yako hiyo tutaweza kufanikiwa kwa sababu mimi naona kabisa ambavyo mimi ninavyoshow love kwako.

Kundi la Makomando Lasambaratika,Kila Mmoja Aamua Kujitegemea.

Makomandoo ni moja ya makundi makubwa ambayo yalikuwa yanategemewa kufika mbali lakini sio kilakinachotegemewa kinaweza kwenda kama kinavotakiwa kuwa, ndivyo ilivyo kwa kundi la makomando ambalo sasa hivi itaaanza kusikika kila mmoja akifanya kazi peke yake na chini ya uongozi wake.

Akithibitisha hilo moja ya wasanii wa kundi hilo Fredy Whine amesema kuwa kwa sasa mwenzake Muki yuko busy nyumbani na mambo yake hivyo kwa upande wake hawezi kusubiria mpaka Muki akitaka kufanya kazi tena.Hata hivyo Fredy Whine nae kwa sasa yuko chini ya menejiment mpya inayomsimamia kazi zake.

Yeye yuko kwake  anafanya kazi zake, siwezi kusubiria amalize mambo yake tufanye wote, na mimi am musician kwaio acha nifanye .tulikutana tukashare ideas kwaio nitafanya.so its not makomando, its me new boy ,unapona mtu yko busy na mambo yake inabidi ufanye yako.Yeye kwa sasa ana familia yake, na mimi nilikuwa nayo na ninayo lakini ya kwake ni ngumu zaidi.

Kuna project nyingi nilikuwa nafanya mwenyewe , kuna wimbo nimeimba nikautoa nikauleta makomandoo sauti yake haipo lakini hakuna aliyejua,Wengi walikuwa wakisema kuwa alikuwa ananibeba lakini sasa hivi ni muda wangu kuwaonyesha kuwa mimi pia ninaweza kuliko.

Nae meneja mpya wa Fredy, Henry Ado Mapunda  anasema kuwa makomandoo ni moja ya kundi alilokuwa akilipenda sana na amesikitika sana kuiskia kuwa wanshindwa kuendelea kuwa wote tena lakini pia anaona bora kumchukua fredy na kufanya nae kazi kwa sasa.

Nilikuwa nawapenda sana makomandoo, nimesikitika sana sana kama wamevunjika na hata aliposema kuwa yuko free nikaona let come together na tufanye kitu pamoja.tuko na ziggy zaggy from Nigeria watafanya kazi kwa pamoja na wiki ijayo Fredy Whine atafanya events Kigali.

Makomandoo walianza muziki wakiwa kundi la watu wanne baadae wawili walikuja kuondoka na kubaki wawili ambao wamekaa zaidi ya miaka 10 pamoja na sasa hivi familia imewatenganisha, wameshindwa kufanya kazi pamoja  kwa sababu Muki sasa hivi ana kabiliwa na maswala ya kifamilia.

Ali kiba, Diamond Wanatumia Ndere-Fredy Makomandoo

Mmoja wa wasanii wa kundi la musiki wa Bongo Fleva nchini  kundi la Makomandoo, Fredy, amefunguka na kusema  kuwa katika miziki wanaoufanya  kuna baadhi ya wasanii wanafanikiwa katika muziki kwa kuboost muziki wao na “ndere” yaani nguvu za giza.Msanii huyo alipoulizwa kuhusu kufanikiwa kwa muziki kuna sababishwa na uchawi alikubali kuwa ndio ni kweli uchawi unahusika na kutaja baadhi ya wasanii, hata hivyo msanii huyo aliambiwa ataje watu watatu lakini akasema kuwa wapo wengi zaidi ya watatu.

“ndere zipo,mi sikatai, mimi mwenyewe natandika ndere” alikiri msanii huyo.Na alipoambiwa ataje wasanii wengine akarudia tena, “mimi mwenyewe ndere,kiba ndere, diamond ndere ‘, alipoulizwa kuhusu kiba akasema “kiba..Alikiba”.

Katika mahojiano na bongo 5 ambapo ndio walipokuwa wanafanyiwa , alikuwepo pia msanii mwingine wa kundi hilo anaejulikana kama muki na yeye alisema kuwa”mafanikio ya mtu yanakuja kutokana na juhudi binafsi, kila mtu kuna jinsi anavyojituma hizo ndo zinaweza kumfanya mtu afanikiwe, lakini ingawa wapo wanaofanya dua na matambiko ..Ila kwa upande wangu huwa ni dua tu, mnaweza kumwita kiongozi wa dini akafanya sala kisha natoa wimbo”alisema Muki.

Wakiwa kama wasanii inawezekana kuna wanachokiona kwa wenzao, na kama kweli kuwa muziki wa Tanzania unafanikiwa kwa sababu ya uchawi basi bado wasanii wanahitaji kufanya jitihada kubwa za kufanikiwa. Wasanii aliowataja ni wasanii wakubwa na wamekuwa pengine mifano kwa wasanii chipukizi katika kutoboza katika sanaa ya  muziki pia.

Makomandoo ni moja ya kundi bora la muziki  ambalo lilianza tangu kipindi cha miaka ya nyuma na wimbo wao uliosikika sana wa’ kibaba baba’ limefanikiwa kukaa kwa muda mrefu katika game bila kuteteleka, yalikuwepo makundi mengi lakini yalishindwa kutunza umoja na kujikuta yanavunjika hii imekuwa tofauti kwa kundi ili ambalo tangu walipoanza  mpaka leo  lakini bado ni kundi la muziki ambalo halina habari za kugombana au kuwa na skendo yoyote mbaya ya kufanya kundi lionekana linafanya vibaya na kwa sasa wanatamba na kibao chao cha “anaona gere”.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.