Karen Gadner Afunguka Baada Ya Picha Kuza Gumzo Mtandaoni

Msanii wa Bongo fleva kutoka THT anayefanya vyema na wimbo wa ‘Lawama’ Malkia Karen ambaye pia ni mtoto wa Mtangazaji wa Clouds Fm Gadner Habash amefungukia picha ili Goleta gumzo Kwenye mitandao.

Siku chache zilizopita Karen aliposti picha Kwenye ukurasa wake wa Instagram iliyomuonyesha akiwa amemuegemea Kwenye kochi Baba yake mara moja ilizua gumzo baada ya watu kudai haikuendana na maadili ya Kitanzania.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Malkia Karen amesema haoni tatizo na ile picha kwani alipigwa na marafiki zake ambao alikuwa nao ndani na hakuwa na maana mbaya kwani anampenda sana Baba yake:

Mimi binafsi sijaona kama ile ni picha mbaya na hata kwa Baba yangu sidhani kama ni picha mbaya .

Lakini pia Malkia Karen aliomba radhi kwa picha ile kama Iliwakera watu:

Ni kweli kila mtu anakuwa na mtazamo wake kwa sababu nikiposti picha watu wakaiona sio vibaya kusikia maoni ya watu na kama kuna watu wamekwazika kwa kuwa wameona kama sio maadili basi naomba wanisamehe Kwa kweli”.

 

karen Aelezea Baba Yake Hakutaka Afanye Muziki, Ataja Mchango wa Jay Dee Kwake.

Msanii chipukizi wa bongo malkia karen amefunguka na kusema kuwa katika kufanya kazi ya muziki alipata upinzani mkubwa sana hapo mwanzo kutoka kwa wazazi wote wawili.karen ambae ni mtoto wa captain g habash anasema kuwa baba yake mara nyingi alikuwa akiogopa sana kuhusu maadili hasa kukaa vizuri sana mbele za watu.

Baraka zote zipo kutoka kwa wazazi wote wawili,mwanzoni ilikuwa ngumu sana kwa wote wawili na pia kwa uapnde wa baba ni kwamba kwa sababu yeye tayari ni nguli katika tasnia ya muziki kwaio alikuwa  anajua, kikubwa alikuwa  anakazania maadili tu,

Lakini pia Karen anakiri kuwa moja ya wat waliochangia sana kufika katika muziki na kufanikiwa ni mama yake mdogo Jay Dee ( ambae alikuwa akiishi na baba yake kwa ndoa) kutokana na kukaa nae vizuri lakini pia alikuwa akimlea vizuri na kumpa ushawishi mkubwa wa kufanya muziki.

Nilishawahi kukaa nae na alinilea vizuri sana hasa katika muziki,Kwakweli alini-inpire sana na katika nyimbo ninazozipenda ni ule wa faraja.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.