Vijana Wawe na Upendo kwa Wazazi wao Kama Godzilla :-Mama Godzilla

Mama mzazi wa marehemu Godzilla amefunguka na kutoa shukurani zake kwa watu wote waliohudhuria msiba wa mtoto wake na kujitoa kwa hali na mali katika kipindi hicho kigumu walichokuwa wakipitia na familia yake.

Mama huyo anasema kuwa Mungu ndie pekee anaweza kuwalipa wale wote walioguswa na msiba  huo  na kuamua kuungana na familia kwa ajili ya umpumzisha mtoto wake.

Hata hivyo mama huyo pia ametoa ushauri kwa vijana  kuwa na upendo na wazazi wao atika kipindi chote cha maisha yao kwa sababu kwa upande wake , alikuwa akipendwa sana na mtoto wake kiasi wamba msiba huo ulimuumiza sana na kumpa kidonda.

Mama anasema uwa God alikuwa mtu wa kumuuliza mama yae kila kitu alichokuwa akifanya na umtaka mama yake kusihi kwa amani na kufurahia kila kitu katika maisha yae na ndio maana hiyo ilimfanya kuumia sana.

Mama Aomba Nyimbo za Mwanae Zipigwe Msibani :-Godzilla

Mama wa marehemu Godzilla ameomba nyimbo za mwanae zipigwe katika msiba huu na kuacha kuweka nyimbo zingine ambazo zingemtia machungu zaidi ya kumkumbuka mtoto wake .

Mama huyo ambae amekuwa mwenye uchungu sana kwa muda wote na kuongea maneno yenye huzuni na huruma kubwa kwa kutokuamini kuondoka kwa mtoto wake anasema kuwa anajua kuwa kuna baaadhi ya nyimbo za mtoto wake  zina maadhi ya dini hivyo anaomba nyimbo hizo zipigwe katika msiba.

Mama anasema kuwa kuna nyimbo ambazo zilikuwa ziko studio bado lakini zilikuwa zinakaribia kutoka kwa sabab tayari mtoto wake alikuwa amesikiliza hivyo anaomaba kuzisikia tena.

Akiongea na waandishi, moja ya watu wa karibu wa God , anasema kuwa mama alikuwa akimwambia alikuwa akipelekwa studio na mwanae na alikuwa akimsikiliza baadhi ya nyimbo.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.