Manfongo Akanusha Kukamatwa na Polisi na Matumizi ya Bangi.

Msanii wa muziki wa singeli nchini manfongo amakanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa katika mitandao kuwa alikamatwa na kuwekwa ndani kwa muda na kusema kuwa wale walikuwa sungusungu ambao waliwakuta sehemu na kuwaomba pesa na walikata kutoa ndipo walipowapeleka kituo cha polisi.

Manfongo anasema kuwa katika eneo walilokuwepo kuna watu huwa wanavuta bangi hivyo walipoona na wao wamekaa maeneo hayo wakahisi kuwa ni kundi moja lakini hata baada ya kuwanusa mikono waliwachukua na kuwaomba ela na walikataa kutoa ndipo waliamua kuwapeleka polisi.

Sikukamatwa na polisi , wale walikuwa ni sungusungu ambao walinikuta maeneo ya Tandale, nilikwenda kwa kaka yangu kusalimia na walipokuja walinikuta tuko ndani na waliamua kutunusa mikono kama tunavuta bangi lakini waliamua kutukama na kutaka kutypeleka kituoni, yulikuwa njiani wakataka pesa na tulipowaambia hatuna wakachukua hatua ya kutupekea polisi.

Lakini pia Manfongo amekanusha taarifa za kua yeye ni mvutaji wa bangi kuwa sio za kweli hata kidogo.

 

Manfongo Achukizwa na Sungusungu .

Msanii wa  muziki wa kisingeli nchii, Manfongo amesema kuwa amekatishwa tamaa sana na ufanyaji kazi wa sungusungu kutokana na kubambikiwa kesi kwa baadhi ya wananchi bila kuwa na makosa yoyote.

Manfongo ameongea hayo alipokuwa akiongea na eNews huku ikiwa imepita siku chache tu tangu aliporipotiwa na baba yake mzazi kuwa msanii huyo aliwekwa ndani kutokana na kosa la kukutwa na bangi.

Sungusungu wa  Ali Maua wamekuwa na tabia mbaya sana wamekuwa wakifanya kazi knyume na utaratibu sana naomba waondolewe tubaki na polisi kama kuna tatizo tutaenda kusema polis tu maana wale sungusungu wanasumbua vijana pamoja na wananchi na wakina mama sana.

Kitu kikubwa alichosema manfongo ni kuwa sungusungu wamekuwa na tabia ya kuomba pesa kila wanapokutana na raia na kama unakuwa una pesa hiyo basi inakuwa kama umefanya kosa na kukamatwa.

 

Man Fongo Akamatwa na Polisi

Baba mzazi wa msanii wa miondoko ya singeli, Man Fongo amedai haelewi sababu iliyosababisha kukamatwa kwa mtoto wake huyo ‘week end’ hii, licha ya kuwa inadaiwa amekamatwa kutokana na kuvuta bangi.

Akizungumza na eNewz, baba mzazi wa Man Fongo amesema yeye alipewa taarifa kuwa mwanaye amekamatwa na madai yakiwa ni kukutwa na bangi japo anajuwa kuwa mwanaye anatumia sigara tu.

“Kuna kitu kinatengenezwa dhidi ya Man Fongo sio bure maana mtu akishakuwa maarufu basi watu hupenda kuwa haribia na kuwachafua kwa baadhi ya vitu. Nilienda kituo cha Polisi cha Ali Maua na nilipofika hapo, nikaulizwa na askari kuwa wewe ndio mzazi wa Man Fongo, nikamjibu ndio kisha yule askari akaniambia mwanao mimi nitamharibia”, amesema baba wa Man Fongo.

Mbali na hilo, baba huyo amesema wakati alipokuwa anakamatwa Man Fongo pia alichukuliwa mdogo wake kwa kile kilichodaiwa kuwazuia askari wasimkamate ndugu yake.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.