Watu Wanafanya Dhambi Makusudi na Kumsingizia Shetani-Martha

Mwanadada Martha Mwaipaja ambae wiki hii alipata nafasi ya kuonekana katika kipindi cha kikaangoni live cha EATV, amefunguka na kusema mengi huku akiwashangaa sana watu ambao wamekuwa wakifanya makosa ambayo wanajua kabisa kuwa ni dhambi lakii wanafanya kwa makusudi .

Martha anasema kuwa watu wamekuwa wakimsingizia shetani kwa amewapitia alkaini uapokuja kuona jinsi dhambi hiyo ilivyotendeka unaona kabisa kuwa watu hao walikuwa wamepanga kufanya kitu hicho.

Kwa kutolea mfano, martha anasema kuwa kuna dhambi kama ya kuzini ambayo imekuwa ikitendwa karibia kila kukicha lakini hata ukiangalia mazingira watu yanayofanyia kityu hicho unaona kabisa kuwa ilikuwa imekusudia huku akisema kuwa kwa nini kama ni shetani amewapitia basi wanaacha kufanya kitendo hicho sebleni na kupelekana chumbani.

Martha amefunguka na kuwashauri watu kubadilika na kmrudia mungu kwa kuamua kutenda matendo yaliyo mema na ya kumpendeza yeye.

Mimi na Mume Wangu Hatugombani kwa Sababu Natambua Majukumu Yangu-Martha Mwaipaja

Msanii wa nyimbo za injili Tanzania martha mwaipaja amefunguka na kusema kuwa wanawake wengi wamekuwa wakishindwa kutulia katika ndoa zao kwa sababu  wanakuwa hawatambui majukumu yao katika ndoa zao.

Martha anasema kuwa kila mtu anamajukumu yake katika maisha ya ndoa na jambo zuri ni pale ambapo watu hao wanakuwa wanaelewa majukumu yao na kuweza kuyatekeleza .akitolea mfano wa ndoa yake na mume wake , Martha anasema kuwa

mimi na mume wangu hatugombani kwa sababu natambua majukumu yangu kama mke, unajua  watu hawajui kuwa kiasili mungu amemuweka  mwanaume kuwa mtawala, amtawale mwanamke  sasa ugomvi mwingi unatokea  pale mwanamke anapotaka kuwa jeuri , kubishana na mwanaume”

Martha anasema kuwa jambo kubwa mwanamke anachotakiwa kujua ni kwamba mwanamke yuko chini ya mwanaume hivyo ugomvi mwingi katika ndoa utokea kwa sababu mwanamke anataka kuwa jeuri na kumbishia mwanaume.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.