Diamond ana Bahati ya Kupata Wanawake wazuri :-Masanja

Msanii na mchungaji na mfanyabiashara maarufu nchini Masanja mkandamizaji amefunguka na kumshangaa sana Diamond kwanini amekuwa akichelewa kuoa kwa sababu mungu amekuwa akimjalia wanawake wazuri  lakini kila siku anakwepa ndoa.

Masanja ambae aliwahi kusema kuwa Diamond anakoelekea atakuja kuoa mganga wa kienyeji kwa sababu ya kuchagua kwake, anasema kuwa anatakiwa sasa aamuae ili aoe kwa sababu kila mwanamke anayempta ni mzuri lakini hajui anakwama wapi.

jamaa amekuwa na bahati ya kupata wanawake wazuri wazuri tu kuna kale kamoja kalikuwa katangazaji sijui ka wapi, mwingine alikuwaga miss lakini siwezi kumsema nmaana sijui yuko wapi sasa hivi, hivi unataka nini kwa mfano au unatafuta chenye AC

 

 

Diamond Atakuja Kuoa Mganga wa Kienyeji :-Masanja

Mchungaji mjasiriamali, Masanja Mkandamizaji  ametoa ushauri kwa Mwanamuziki Maarufu nchini, Diamond Pltanumz kuoa mapema kwani akichelewa anaweza kuoa mganga wa kienyeji.

Masanja amesema kuwa watu wajiulize kila mtu anayetaka kuolewa na Diamond anasema mara analoga familia, hivyo amemtaka kuoa mapema ili kuepuka kuja kuoa mdada anayenuka mitishamba.

Diamond Platnumz oa mapema utakuja kuoa mganga wa kienyeji, wewe jiulize hivi kama wewe huoi sasa hivi nimesikia kila mdada anayetaka kuolewa leo na Diamond nimesikia eh wananiloga na wanaloga familia kama mdada wa kwanza unaenda naye alafu humuoi, pili nae humuoi, watatu mwisho wa siku utaoa kadada kanako nuka mitishamba, Oa mapema ndugu yangu unangoja nini?, Masanja ameiambia Wasafi Tv
Diamond Platnumz kwasasa anatoka kimapenzi na Natasha kutoka nchini Kenya, ambapo mpaka sasa haijajulikana kama atamuoa mrembo huyo.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.