Hata Fid q Anafanya Kiki Katika Muziki-Master Jay

msanii Fid Q akiwa na moja ya tuzo za heshima alizopata hivi karibuni.

Aliyewahi kuwa nguli wa utayarishaji wa muziki nchini, Master Jay maefunguka na kudai kuwa wasanii wenginchini wamekuwa wakifanya kazi kwa vurugu na mbwembwe tu na wala sio kama zamani walivyokuwa wakifanya kazi wao.

Master Jay ambae anasisitiza kuwa wasanii wa sasa wamezoea sana kufanya kazi kwa kiki bla hivyo muziki wao hauendi, anasema kuwa hata msanii mkongwe wa hip-hop Fid qQpia anafanya kazi kwa kiki na ndio maana aliamua kukubali kufanya kazi ya fresh remix.

Wasanii wengi wa sasa wanafanya kazi kwa vurugu vurugu tu ili waachie ngoma pya, hata fid q anafanya kiki tu na ndio maana alikubali kufanya wimbo  wa kiki  ule wa fresh remix

Ikimbukwe kuwa Master Jay alikuwa ni moja wa watayarishaji mashughuli katika bongo fleva na kusaidia kutoa watu wengi sana ambao historia yao ya muziki ilianzia kwa mtayarisahji huyo, lakini pia Master Jay ni moja ya wakongwe walioweza kufanikisha muziki kufika hapa ulipo akiwa kama mwalimu.

Mabinti Zake Master Jay Wamfanya Aache Muziki.

Aliyewahi kuwa mtayarishaji bora wa muziki bongo na kufanya kazi na wasanii wengi na hata kuibua vipaji vya wasanii weng nchini, Master J amefunguka na kutoa sababu kubwa ya yeye kuacha muziki na kuamua kufanya kazi nyingine ili kuendelea kuangalia na kuitunza familia yake.

Master J anasema kuwa kama angeamua kuendelea kufanya kazi ya muziki kama watu walivyokuwa wakimuomba basi hasingeweza hata kuitunza familia yae na kutoa ada kwa ajili ya mabinti zake.

niliacha hii kazi ya ku-produce muziki  sio kwamba nilishindwa ila nilikuwa na malengo,kama ningeendelea ningeshindwa hata kumlipia ada binti yangu. 

Inasemekana kuwa Master J ambae amekuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanadada shaa kwa zaidi ya miaka mitano sasa , ana watoto wakike wa tatu.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.