Aliyewahi Kuwa Mpenzi Wa Mbasha Achumbiwa.

Mwanadada aliyewahi kushiriki Miss  Tanzania mwaka 2008 Jackline Chuwa maarufu kama Jack ambae aliwahi kuripotiwa kuwa aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki wa injili Emmanuel mbasha  amechumbiwa na moja ya wachungaj maarufu huko mkoani Moshi .

Mwanadada huyo ambae aliwahi kuwa katika penzi zito na msanii huyo  amethibitisha hilo na kusema kuwa amechumbiwa hivi karibuni na mchungaji mmoja wa kanisa la kilokole huko Kilimanjaro na wanategemea kufunga ndoa.

Alipotafutwa mrembo huyo alithibitisha hayo kwa kusema “Ni kweli nimechumbiwa na nitaolewa hivi karibuni,jina la mchumba wangu siwezi kulitaja kwa sababu ni mchngaji na kimaadili hairuhusiwi.”

 

Mimba ya Agnes Bado Yamuumiza Kichwa Mbasha

Msanii wa nyimbo za injili, Mabasha  bado anaandamwa na skendo ya kutembea na mwanamitindo Agness na kumpa ujauzito ingawa kwa nyakati tofauti msanii huyo amekuwa akikanusha wao kuwa na mahusiano  nahata kumpa ujauzito mwanamitindo huyo.

Mbasha anasema kuwa yeye na agness hawajuani zaidi ya yeye kujua kuwa mwanamitindo huyo amekuwa kama shabiki yake na yeye amemjua kupitia mitandao ya kijamii tu.Mbasha amesema kuwa  tetesi zinazosambaa juu yake hazina ukweli wowte na hawajawahi kuwa na ukaribu huo.

Agness namjua kama shabiki yangu kupitia kitandao ya kijamii tu,sasa sijui mambo yamegeuka vipi mpaka kufikia hatua ya kuambiwa kuwa mimi nina mahusiano nae.sijawahi kuwa na mahusiano na agnes wala kuwa na kitu chochote kinachoashiria mapenzi.

Sitegemei kupata nae mtoto kama watu wanavyosema kwa sababu sijawahi kuwa na mahusiano na mwanadada huyo,sina mahusiano nae huyo dada ni shabiki yangu tu.-Alisema Mbasha alipokuwa anaongea na Enews ya EATV.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.