Mboso Asikika CLOUDS Fm

Msanii kutoka katika kundi la WCB amesikika kwa mara ya kwanza tangu Clouds media ilipoacha kucheza nyibo zao siku nyingi zilizopita ingawa swala jilo halikuwa limetangazwa public.

Wcb na Clouds wamekuwawakionekana kuwa na mgogoro wa chinichini ingawa hakuna anaetaka kushughulika na swala hilo lakini ni kwa muda mrefu media iyo imekuwa hainachzi nyimbo za wasanii hao kutoka katika kundi hilo.

Jambo la kushangaza ni hapo siku ya jana wimbo wa hodari wa mapnzi wa Mboso kutoka katika kundi hilo pendwa kusikika ukipigwa katika clouds fm huku watangazaji wake wakihusifia kwa nguvu wimbo huo.

Sio dhambi kwa kitendo icho lakii imani ya mashabiki ni kwamba yaliyokuwa chini ya kapeti kati y pande hizo mbili yataisha taratibu.

Nikitoa Ngoma Anakufa Mtu :Mboso

sanii kutoka kundi la wcb, Mboso amefunguka  na kuelezea kwa undani juu ya changamoto na mafanikio aliyoyapata kwa mwaka huu huku akisema kuwa  umekuwa mwaka wa neema kwa sababu ya nyimbo zake lakini upande mwingi kunakuwa na tatizo.

Mbosso amesema kuwa mwaka jana alikuwa na mkosi kwani kila alivyoachia video ya ngoma mpya, siku hiyo hiyo kulitokea msiba mkubwa Tanzania.

Kuna vitu vilikuwa vinatia unyonge. Mwaka 2018 kuna watu walikuwa hawajajua kwamba kila nikitoa wimbo, lazima utokee msiba. Kila nikitoa wimbo, kila nikiweka video. Nakumbuka kipindi natoa Nadekezwa kulitokea Msiba wa mtoto wa dada mmoja anaitwa Muna. Kipindi nakuja kutoa Nipepee kulitokea msiba wa mzee Majuto. Nilivyotoa Hodari kulitokea ajali ya MV Nyerere, nikawa nawaza kwanini zinatokea changamoto kama hizi? ilinipa stress sana.“ameeleza Mbosso kwenye mahojiano yake na Mseto East Africa.

Kwa upande mwingine, Mbosso amesema mwaka huu amejipanga kufanya kolabo na Sauti Sol na kuachia kolabo yake na Mr Flavour.

 

Mashabiki Wabadilisha Muonekano wa Mboso.

Msanii Maromboso amefuguka na kusema kuwa kwa sasa amekuwa na kazi kubwa sana ya kubadili muoneknao wake kwa sasa  ya mashabiki zake ambao wanasapoti muziki wake.

Maromboso amba kwa sasa amekuwa akifanya vizuri kila kukicha kutokoana na kazi nzuri anazofanya na nyimbo mpya anazotoa kila siku anasema kuwa imembidi kubadilisha vile anavyoonekana.

Maromboso anasema kuwa watu wengi walikuwa wakimshauri kuwa amekuwa akionekana kama walimu hivyo ilimlazimu kubadili muoneknao ili kuendana na haiba ya mwanamzuki.

Akiongea na mwandishi , maromboso anasema “Nimebadili muonekanao kwa sababu watu wengi wamekuwa wakiniambia kuwa nimekuwa nikionekana kama teacher”

Mboso Awaonya Wanaomfananisha na Aslay

Msanii Mboso kutoka katika kundi la WCB  amefunguka na kuwaonya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimfananisha na msanii mwenzake Aslay ambae  amkuwa akifanya muziki kwa kujitegemea tangu kuondoka kwa kundi lao la ya moto.

Mboso anasema kuwa hawezi kufafanishwa na Aslay kwa sababu Aslay alianza muziki kabla yake na kabla hata ya kuundwa kwa kundi walikuwa wakifanya kazi hivyo hawawezi kulingana katika hilo.

hakuna kitu ninachokiona alafu nikajisikia vibaya kama ninapoona ninafananishwa na Aslay, yuke mimi ni kaka yangu na isitoshe mimi nimeanza music kama solo artist nikiwa na miezi 9 tu lakini yeye kaanza muziki tangu mwaka 2011.Ukinifananisha nae unakuwa unamvunjia heshima yake.

Mboso , Aslay na wasani wengine wawili walikuwa wakifanya kazi katika kundi moja lakini baada ya kundi hilo kuvunjika kila mmoja alianza kuimba kama msanii wa kujitegemea huku Mboso akisajiriwa na WCB kuwa chini yao.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.