Mama Natasha Atoa Siri Nzito Kuhusu Monalisa

Uhusiano  waliona kati ya Mama Natasha na mtoto wake wa kike Monalisa umekuwa ukiwatamanisha watu wengi kuwa na mahusiano hayo mazuri na watoto wao, kuna muda utashindwa kugundua kuwa wawili hawa ni mtu na mtoto wake,ukiachana na urafiki lakini pia wote wamekuwa wakifanya azi katika tasnia moja na hii inaweza kuwa ni chachu ya upendo wao kuwa mzuri zaidi.

Hivi karibuni Monalisa aliweka bayana katika ukurasa wake wa instagram juu ya siri nzito ambayo mama yake hakuwahi kumwambia tangu amemuweka Duniani lakini siri hiyo ilitajwa kwa mara ya kwanza waliokuwa katika mahojiano ya radioni katika kituo kimoja cha radio.

Juzi katika mahojiano ya dizzimonline mama yangu aliamua kusema siri ambayo hakuwahi kuisema  kabla  na mimi ndo nikaisikia hapo, kwamba wakati yeye ni mjamzito  alikuwa mdogo sana na hivyo alishawishiwa sana na familia yake kuitoa mimba yangu ili aweze kundelea na masomo na maisha yake kwa ujumla lakini ALIKATAA na leo hii anajivunia mimi.

nimewaza sana mama angenitoa tumboni, ingekuwaje? ina maana nisingekuwepo Duniani kabisa, au ningezaliwa na mama mwingine nina maswali mengi na nimekosa majibu lakini nimepata sahihi moja tu kuwa WAMAMA MSITOE MIMBA WALA KUTUPA WATOTO.no matter upo katika hali gani  tunajua kabisa kuwa wababa ni changamoto sana  anaweza kukubwaga na ujauzito wako na ukajuta na dunia lakini kwanini utoe? you never know umebeba nani.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.