“Moni Hapendi Niwe na Mabifu Mtandaoni”- Nai

Video vixen maarufu kwenye tasnia ya Bongo fleva Nai amefunguka na kuweka wazi kuwa mpenzi wake ambaye ni staa wa Hip hop nchini Moni Centrozone hapendi akiona ana mabifu kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Nai alisema huwa analazimisha tu kuwajibu wanaomsema vibaya mitandaoni, lakini ukweli ni kwamba mpenzi wake huyo hapendi na amekuwa akimkataza mambo hayo mara kwa mara.

Katika vitu ambavyo mpenzi wangu Moni hapendi ni mimi kuwa na ugomvi na wenzangu hasa mitandaoni. Huwa anakereka sana na mara nyingi amekuwa akiniambia nikae kimya, lakini kuna wakati nashindwa kuvumilia matusi na maneno mabaya ambayo nakuwa naambiwa na baadhi ya watu wasiopenda maendeleo yangu, hivyo najikuta nimewajibu ili na mimi nafsi yangu iridhike”.

Siku chache zilizopita Nai aliingia kwenye Bifu kali na video vixen wengine kama Mke wa Rayvanny maarufu kama Fahyvanny na rafiki yake Official lynn.

Moni na Nai Waamua Kurudiana Rasmi

Msanii wa Bongo fleva nchini anayefanya miondoko ya Hip Hop Moni Centrozone amerudisha majeshi yake kwa mpenzi wake video vixen Nai.

Wiki kadhaa zilizopita Moni na Nai walisikika sana Kwenye Media mbali mbali wakirushiana maneno baada ya kuachana ambapo kulikuwa na tuhuma nyingi kama vile michepuko.

Nai alimtuhumu Moni kwa kumpiga na hata kudai ana michepuko mingi akiwemo mmoja wa marafiki wa Gigy Money.

Kwenye Interview na Wasafi Tv Moni na Nai wamethibitisha kurudiana na kuweka wazi kuwa wameamua kuweka tofauti zao pembeni:

Kwa sasa tupo sawa lakini haya ni mambo ya ndani japo kuna kukosana na kuelewana lakini siri zetu za ndani ambazo tunajua wenyewe tunamalizana vipi”.

Wapenzi hao waliweka wazi kuwa ni jambo la kawaida katika mapenzi kugombana na kwa kuwa wanapendana hivyo wameamua kurudiana.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.