Dudubaya: Mr. Nice Hana Tofauti na Dr.Shika Anajiona Tajiri Kumbe Hamna Kitu

Mwanamuziki mkongwe wa mziki wa Bongo fleva, Dudubaya ameibuka na kudai kuwa mkongwe mwenzie msanii aliyetamba miaka ya nyuma Mr. Nice sio mzima kabisa bali ni mgonjwa mahututi.

Mr. Nice amelifufua upya bifu lake na Dudubaya baada ya kudai kuwa amefulia na anahitaji msaada na kama hatojirekebisha atamchukua na kumsaidia maneno ambayo yamemuuzi hasimu wake Dudubaya.

Dudubaya Alipohojiwa na kituo cha televisheni cha East Africa kuhusiana na tuhuma hizo alizorushiwa na hasimu wake wa siku nyingi Mr. Nice, Dudubaya amefunguka na kumjibu kuwa Mr. Nice hana uwezo wa kumsaidia yeye mkwanja na pia yeye nmgonjwa mahututi anayehitaji msaada wa maombi kutoka kwa mchungaji Gwajima ama Mama Rwakatale au mzee wa Upako lakini pia Dudubaya amemfananisha Mr. Nice na Dr. Shika kuwa anajiona ana hela kumbe hamna kitu.

Mr. Nice ana kauli za kuchekesha kwa sababu mgonjwa mahututi hawezi kumsaidia mtu ambaye ana afya kama Mimi,namfahamu vizuri Mr. Nice ndio maana ninasema ana hali mbaya kiafya mpaka kiuchumi hapo alipo ameathirika kisaikolojia ndio maana bado anaota maisha yake alioishi kipindi kile staa na hata pesa alizopata kipindi kile ndio maana namfananisha na Dr. Shika aloyekuwa na hela kipindi hiko Urusi lakini mpaka Leo anaota anadhani bado zipo kwaiyo hapo unaweza ukaona mfanano Kati ya Dr. Shika na Mr. Nice”.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.