Mama Watoto Wangu Ananivumilia sana :-Msami

Msanii wa muziki nchini msami amefunguka na kusema kuwa msimu huu wa siku ya wapendanayo amekuwa akiwaza na kujitahidi sana kutaka kurudisha mapenzi kwa mama wa watoto wake kwa sababu amekuwa mama bora kwa mtoto wake lakini mwenye uvumilivu sana kwake.

msami anasema kuwa pamoja na kwamba kuna muda anakuwa mbali nae lakini amekuwa akimjali na kuheshimu sana hisia zake na kazi zake pia, anasema kuwa mama huyo ni mwanamke anaeamini kuwa anampenda kutokana na mapenzi yake.

msimu huu n wa muhimu sana kwangu kwa sababu nataka kufanya kitu kwa mama wa watoto wangu, ananipenda, ananijali na kunisikiliza sana, ananikubali kwa kila hali na kukubaliana na yale tunayoyapitia kila siku.kwa upande wangu natumia siku hizi kuzidishia mapendo.

Msami Aongelea Kurudiana Kwa Rihana na Chris Brown

Siku chache zimepita tangu katika ukurasa wa mwanadada Rihana kuonekana kuna comments ya msanii Chris Brown akisifia jambo fulani kuhusu picha aliyokuwa ameweka na vazi alilokuwa amevaa.

watu walianza kuhoji kuwa inawezekana wawili hao kwa sasa wamekuwa na mahusiano ya karibu au hata wanataka kurudisha mapenzi yao tena kama zamani hata kama waliwahi kugombana na kuingia katika mgogoro mkubwa ?

Wila mtu aliongea lake,lakini moja ya wasanii wa bongo fleva nchini msami alipata nafasi ya kuongea na watangazaji wa clouds medai na kuulizwa swala hilo akiwa pia na yeye ni moja ya watu waliowahi kuwa na mahusiano na mwanadada maarufu bongo.

Msami anasema inawezekana hakuna hata nia ya kurudiana kati yao lakini tu kuweka maoni katika ukurasa wa mpezi wako wa zamani hilo ni jambo la kawaida tu.

kucoment kwenye ukurasa wa mpenzi wangu wa zamani ni jambo la kawaida tu wala sio kama kuna kitu cha ajabu hapo.

Kuwa na Mademu Wazuri Kwangu ni Kawaida :-Msami

Msanii wa bongo fleva nchini ,Msami amefunguka na kusema kuwa kwake kuwa na mademu wazuri ni kitu cha kawaida ingawa watu wamekuwa wakisema kuwa tangu ameachana na Uwoya amekuwa hana umaarufu tena.

Mwanamuziki huyo ambae kwa sasa hasemwi sana kama ilivyokuwa hapo awali , anasemwa kupata umaarufu, kiki na jina sana pale alipokuwa na mwanadada kutoka bongo movies Irene Uwoya.

Hata hivyo yeye mwenyewe anakanusha swala hilo na kusema kuwa katika maisha yake kuwa na wasichana wazuri ni kitu cha kawaida ila tu sio kila kitu mpaka utoe taarifa kuwa kinafanyika.

Wakati mwingine sio lazima kila kitu ukiweke katika mitandao, mimi nina bahati ya kuwa na watoto wazuri tu kikitoka kitu kinaingia kitu kuwa na mademu wazuri kwangu ni kawaida”

Msami Ajuta Kutembea Na Uwoya,Alishawahi Kukutana Na Ndikumana.

Msami ni mmoja wa wasanii wa bongo fleva wanaofanya vizuri katika kuimba na kucheza pia,lakini pia msami ni moja ya wanaume wanaosemekana kuwa na uhusiano na Irene Uwoya kipindi ambacho Irene alikwa tayari ameshafunga ndoa na Ndikumana.

Akiongea na mwandishi kutoka Millard ayo, Msami anakiri kuwa alikuwa na uhusiano na Irene Uwoya lakini alipouliza mahusiano hayo alimbiwa kuwa wameshagombana, lakini baaada ya kufatilia sana alikuja kuona kuwa wawili hao hata kama wamegombana lakini bado wapo katika ndoa na kwa maadili ya dini ya kikristo ndoa hiyo haijavunjika.

Lakini pia Msami anasema kuwa hata baada ya kugundua kitu hicho aliongea na Irene na kumuomba waachane ili awe huru kwa sababu nafsi yake ilikuwa ikimsuta kwa kitendo hicho cha kutembea na mke wa mtu.

Msami anasema kuwa alishawahi kukutana na Ndikumana mara moja uwanja wa ndege, na hakuwahi kuwa na bifu nae na hata alipopata taarifa za msiba aliumia sana na kuonyesha hisia zake alimpigia Irene Uwoya na kumpa pole ingawa hawakuweza kuelewana vizuri sana hivyo pia aliamua kumpost Ndikumana instagram aktika ukurasa wake kama njia ya kuonyesha kuguswa kwake.

Katika kuongezea kwake ,Msami anasema kuwa hawezi kujua mpaka Ndikumana anafariki alikuwa anawaza nini kuhusu yeye lakini anachoamini kuwa yeye aliongea na mungu wake kuhusu dhambi aliyotenda ya kutembea na mke wa mtu na anaamini atasameheka.Akiendelea kwa kutoa ushauri Msami anasema kuwa kwa kipindi hiki kigumu Irene anachopitia inabidi awe mvumilivu na wala hasiskilize maneno ya watu, lakini aangalie jinsi ya kumlea mtoto wake wa kiume aliempata na Ndikumana na kumpa malezi bora maana maneno katika mitandao huwa yanaishi hivyo mwanae atayakuta.

Mimi na Ndikumana tulishakuta mara moja airport alikuja kutupokea,na tulisalimia vizuri tu na kitu kikubwa watu wanatakiwa kujua upaswi kumpenda mtu akiwa amekufa au amepata matatizo , nilifurahi kwa kile alichokifanya Hamisa kwa Lulu.

Nilikuwa naheshimu sana ndoa ya Irene na Hamad, na nilikuja kujua nimefanya makosa kutembea na Irene, na sababu kubwa ya kuachana na Irene ni baada ya kugundua kuwa ni makosa kutembea na mtu aliyefunga ndoa na bado hajaachana na mumuwe, hivyo nilimwambia Irene ni bora tuachane.Mimi ni mkristo na dini yetu hairuhusu hivyo

Kwa Irene wapo watakao mbeza na wapo watakao mfariji hivyo azingatie wale watakao mtia moyo tu kwa kipndi hiki, na kujua ni jinsi gani ya kumlea mwanae maana maneno ya mitandao yapo na atakuwa atayakuta. -Alimalizia Msami

 

Mrembo Aliechora Tatoo Ya Msami Afunguka

Mwanadada ambae alipata umaarufu mkubwa siku za nyuma kutokana na kuwa na mahusiano na msanii wa kisingeli Dullah makabila, na baadae kuingia katika ugomvi na Husna Sajenti baada ya kuachana msanii huyo huku chanzo kikisemekana kuwa ni mwandada Husna. Ameamua kufunguka kuhusu mahusiano yake na msanii Msami Baby na kuhusu swala la yeye kuchora tatoo yenye jina la msanii huyo.

Wiki iliyopita msanii wa muziki anayefanya vizuri katika kuimba na kucheza pia Msami, aliongea kuwa yeye hana mahusiano na msichana yeyote kwa sasa na kama atakuwa na mahusiano angeyaweka wazi lakini amekuwa akimjua msichana huyo anaeitwa Asali na amesikia kuwa amechora tatoo ya jina lake lakini hana mahusiano nae yoyote isipokuwa wanafahamiana kwa kwasababu anakaa karibu na  nyumba ya mama yake.

Akiongea na eNews ya EATV, mwanadada Asali amekiri kweli kuwa amechora tatoo lakini kama shabiki tu na rafiki wa karibu wa msanii huyo kwa sababu wanakaa mtaa mmoja  na amekuwa akipita kwao mara kwa mara, lakini pia ni rafiki yake anaempenda na kumkubali  kama shabiki”Ni rafiki yangu, nampenda namkubali,napenda muziki wake,napenda hata anavyokatika lakini kitu cha kushangaza nimeona juzi anaongelea mambo yale, hakupaswa kuongelea mambo yale kabisa kwa sababu hata mimi siwezi kuwa nae na sijawaza kuwa nae” aliongea Asali

Asali ambae mara ya kwanza alikuwa na mahusiano na msanii Dullah Makabila alipoulizwa kati ya Dullah Makabila na Msami ni mwanaume gani anaenjoy akiwa nae aliitika na kusema kuwa akiwa na Msami ana-enjoy zaidi ilihali mara ya kwanza alikataa kuwa hana mahusiano yoyote na Msami wala hana hisia nae.

Asali alisema kuwa kwa sasa hana mahusiano na mtu yoyote lakini kitendo cha Msami kumwambia kuwa hawezi kuwa nae kwenye mahusino kimemkera kwa sababu hajui maneno hayo yamtokea wapi ilihali hata yeye pia hakuwahi kuwaza kuwa na mahusinao nae zaidi ya kuwa marafiki  na kuwa anamkubali kama shabiki wake.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.