Muigiza Maarufu Bongo, Muna Love, amezungumza na waandishi wa habari leo nyumbani kwake maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam na kuweka wazi jinsi ambavyo alikutana na Peter Zakaria Komu, mwanaume ambaye hivi karibuni ilisemekana kuwa ndiye baba wa mtoto wake Marehemu Patrick.
Muna anasema kuwa kipindi anakutana na peter tayari alikuwa mjamzito wa mimba ya Casto Dickson,lakini akiwa katika ndoa alikumbana na baadhi ya mambo yaliyomfanya kauchika katika ndoa akiwa tayari amshafanya mambo mengi na peter kama baba wa mtoto wake.
“Nilikutana na Peter jijini Mbeya tukiwa tunafanya kazi Safari Pool Table, tulikaa kwenye mahusiano kwa miezi miwili tukaingia kwenye ndoa, lakini kuna vitu nilivyokutana navyo kwenye ndoa hiyo nikaamua kuachika.
Wakati naingia kwenye mahusiano na Peter nilikuwa nina mimba ya Casto ya miezi miwili, Casto aliikana mimba hiyo. Baadaye alirudi wakati mtoto Patrick akiwa na miaka mitatu. Kwa sababu nilizaa nikiwa kwenye ndoa na Peter ndiye alisimamia hata ubatizo ndizo picha zilizosabaa, lakini hata yeye Peter anaujua ukweli kuhusu mtoto huyo.
“Tulifanya taratubu na Casto za kubadilisha jina la mtoto pale RITA lakini kuna ugumu uliotokea, lakini tulikuwa tunaendelea kufuatilia,” amesema Muna