Mwana FA Amwagia Misifa Kibao Lady JD

Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Hamidaa Mwinjuma maarufu kama Mwana FA amejikuta akimwaga Misifa lukuki kwa msanii mwenzake mkongwe Lady Jay Dee baada ya kushuka kwenye steji moja waliopiga shoo.

Weekend iliyopita Jay Dee alipiga bonge moja la shoo kwenye Ukumbi wa Police Officers Mess uliopo Oysterbay jijini Dar na Mwana FA amemsifi  Jay Dee kuwa ameonesha ukakamavu kuandaa shoo mwenyewe bila kutegemea promota.

Mwana FA na Jay Dee walikuwa maadui wa kutupwa kwa kipindi cha miaka mitano huku sababu ikidaiwa kuwa ni kugongana kwenye shoo kwa siku moja lakini wawili hao walimaliza tofauti zao hivi karibuni na kila mmoja kumposti mwenzake kwenye mitandao ya kijamii.

Katika usiku huo, Lady Jay Dee  alimkaribisha  jukwaani Mwana FA na kuimba naye baadhi ya ngoma walizotamba nazo ambapo walikumbushia Ngoma ya Msiache Kuongea na Hawajui huku shangwe zikiwa za kutosha jukwaani ‘kutoka kwa mashabiki zao.

Kwenye Interview aliyofanya na The Showbiz, mara baada ya kushuka jukwaani, FA alianza kwa kumfagilia JayDee;

Wasanii wakubwa kiwango cha Lady JayDee walitakiwa kuwa na shoo zao siyo kutegemea mapromota wawaandalie, kwa hiyo kitu kilichonivutia kwake na kuamua kumsapoti ni kitendo cha kuandaa shoo mwenyewe”.

 

Mwana FA Amefunguka Kuhusu Message iliyompatanisha na Jay Dee

Mwanamuziki mkongwe wa Bongi fleva, Mwanafalsafa ‘Mwana FA’ amefunguka na kuongelea bifu lake lililokuwepo baina yake na msanii mwenzake mwanadada Lady Jay Dee na jinsi ujumbe mfupi wa maneno ulivolimaliza bifu hilo.

Bifu la Jay Dee na Mwana FA lilianza kipindi korefu kidogo nahisi ni moja kati ya bifu refund katika mziki wa Bongo fleva. Ingawa hawakuwa na bifu siku zote kwani mwanzoni walikuwa marafiki na kuna ngoma kibao kali za zamani walizotoa zilizofanya vizuri lakini bifu lao lilisababisha uhasama mkubwa mpaka kupelekea kugawanya mashabiki huku kila mmoja alienda upande uliompendeza kwa wakati huo.

Jay Dee na Mwana FA walikuwa mahasimu wakubwa lakini kwa sasa wamepatana na jambo hilo liliwapa furaha mashabiki wao lakini Mwana FA ameweka wazi kuwa katika kupatana kwao hakuna mtu aliyemuomba msamaha mwenzake ili kumaliza bifu lao wala hakuna mtu aliyewakalisha chini kama mabifu Mengi ya mastaa yanavyomalizwa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv Mwana FA amesema ugomvi wao wamuda mrefu waliumaliza kwa ujumbe mfupi wa maandishi.

Yaani mimi na Jide hakuna aliyemuomba mwenzake msamaha, mimi ndio nilinza nilimtumia meseji nikamwambia oya vipi? Akajibu fresh, nikamwambia FA hapa usiku nilikutafuta, akajibu Mimi siku hizi nimezeeka nalala mapema ndio hapo maongezi yakaendelea kama kawaida na bifu likaisha mambo mengine yakaendelea”.

Tangu wamalize tofauti zao Jide na Mwana FA wameonekana wakisapotiana katika kazi zao mbali mbali kama Jide alivyotoa nyimbo yake mpya MwanaFA alimsapoti kwa kuitangaza kwenye Instagram yake lakini hivi karibuni wameonekana wakiwa studio pamoja.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.