Mwanaheri Akanusha Kuacha Sanaa Baada ya Ndoa

Mwanamaigizo na mcheza filamu bongo, Mwanaheri amefunguka na kuongelea tetesi zinazosambaa na kusema kuwa amepigwa stop kufanya kazi za sanaa na mume wake Khamis baadaya kumuoa, mwanadada huyo amefunguka na kusema kuwa habari hizo sio za kweli na wala hajaachana na kazi za sanaa.

Akiongea na mwandishiwa habari, Mwanakheri anasema kuwa alishazisikia habari hzio katika mitandao lakini hazina ukweli wowte kwa sababu mume wake amekuwa akiipenda sana kazi yake hivyo hawezi kumzuia kufanya kazi hiyo.

Mimi mume wangu anaheshimu sana na kuipenda sana kazi yangu kwaio kamwe hawezi kukaa na kunizuia kuifanya kazi hiyo,bado naendelea na sanaa wala ndoa hainizui kitu.

 

Mwanaheri Ampongeza Naibu Waziri wa Habari Sanaa na Michezo.

Mwanamaigizo anaefanya vizuri katika tasnia na kazi yake Mwanaheri amefunguka na kumpongeza sana Naibu Waziri wa Sanaa , Habari na Michezo Mh .Juliana Shonza kwa kitendo chake cha kuwafungia na kupiga marufuku uvaaji wa nguo mbaya katika kazi za sanaa kwa wasanii wote wa maigizo na muziki kwa sababu zinavunja maadili ya Tanzania.

Mwanaheri anasema kuwa kitendo cha Naibu waziri kukataza uvaaji wa nguo chafu utasaidia kurudisha hadhi ya sinema za bongo movies nchini kwa sababu wasichana wengi walikuwa wakikosea sana kufanya hivyo.Mwanaheri anasema kuwa wasichana ho wamekuwa wakishusha hadhi ya bongo movies kwa sababu wengi wao wamekuwa wakifanya hivyo na kusababisha watu wengi kutopenda kuangalia movie zao, hivyo anamshukuru sana Mh Naibu waziri.

Sijawahi kuvaa nusu utupu, na wala sidhani kama itatokea,ninaipongeza sana serikali kwa kitendo chake cha kukataza mavazi kama hayo na picha za nusu utupu zilizokuwa zikiwekwa katika mitandao na wasanii kwa sababu kwanza zinaharibu maadili ya kitanzania,ninachoamini kupitia ili hadhi ya bongo movies na filamu itarudi kwa sababu jaii ilitudharau kutokana na mambo hayo.

Hivi karibu kuna baadhi ya wasanii wamepata adhabu baada ya kuwa na tabia ya kuvaa na kuweka picha za utupu katika mitandao ikiwa ni moja kati ya hatua kubwa zinazofanywa na serikali kwa ajili ya kuzuia uharibifu wa maadili unaofanya na wasanii ambao wamepewa dhamana ya kuwa vioo katika jamii tunazoishi.

 

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.