Ustar Wangu ni Nje ya Ndoa. :-Mwanakheri

Mwanadada Mwanakheri amefunguka na kusema kuwa katika maisha yake ya uigizaji amekuwa akifanya ustae nje ya nyumbani kwake lakini akifika nyumbani kwake yeye ni mke wa mtu na wala sio staa tena.

Mwanakheri anasema kuwa mara nyingi amekuwa akijikumbusha kuwa endapo ataleta ustaa nyumbani inaweza kumharibia nyumba na familia yake na hata kuvunja ndoa kwa ujumla hivyo kila siku amekuwa akifikilia hilo.

Mwanakheri anasema kuwa amekuwa akijifunza inavyotokea kwa mastaa wengine na anaona kuwa kwake haiwezi kutokea kwa sababu mara zote amekuwa makini na swala hilo.

kikubwa ni kuwa nikimuomba sana Mungu kuhusu kuilinda ndoa yangu, lakini kikubwa pia ni kwamba niekuwa nikimheshimu sana mume wangu, nampenda na ninamhshimu sana na hivyo maisha yangu ya ndani ya ndoa ni tofauti na ya huko nje kabisa.

Mwanakheri Afunguka, Tofauti na Sanaa Yeye Pia Ni Machinga.

Msanii wa bongo movie, Mwanakheri amefunguka na kusemakuwa pampoja na kwamba yeye anafanya kazi za sanaa lakini pia kazi anazofanya nje ya sanaa zimekuwa zikimsaidia sana kuendelea kujikimu na kuweza kumudu maisha yake binafsi.

Mwanakheri anasema kuwa kama angekuwa amekomaa tu katika sanaa bila kuwa na kitu kingine wala hasingekuwa hivyuo alivyo .mwanakheri ambae kwa sasa amefungua duka kubwa  la kuuza nguo ainaya madela tandika anasema kuwa umachinga huo ndio uliomuokoa na kumuweka mjini kwa sasa.

Mimi ningefanya haya wala nisngekuwa nimefika hapa hata kidogo lakini kwa sababu niliweka mambo ya ustaa pembeni na  kuamua kufanya maisha na mpaka sasa mungu kanibariki, siwezi kusema kuwa nitakosa ela ya kula hata kidogokama ningesubiri mpaka filamu zangu ziuze ningekuwa katika wakati mgumu sana.

 

Siri Imevuja, Mwanakher Aolewa Mke wa Pili.

Wikiend iliyopita kulisambaa kwa picha za mwanadada Mwanakheri  anaefanya vizuri katika tasnia ya movies bongo kuwa amefunga ndoa huku ikisemekana kuwa sio watu wote waliokuwa wanajua kuwa mwanadada huyo ameolewa mpaka picha zilipoanza kusambaa.Sasa siri imekuja kujulikana kuwa mwanadada huyo aliamua kufanya kwa siri kwa sababu mwanaume aliyemuoa ni mue wa mtu na mwanaume huyo hakutaka mke wake kujua swala hilo la ndoa.

Chanzo cha habari hii ambae ni mtu wa karibu wa Mwanakheri alipokuwa akiongea na Global Publishers alifunguka na kusema kuwa mwanaume aliemuoa Mwanakheri ni mume wa mtu na ba awa familia yake na watoto na ni moja ya wafanyabiashara wakubwa bongo.

kama hamna ubuyu ni kwamba mwanaume aliyemuoa anandoa na watoto na ndio maana aliamua kufanya kimyakimya bila ya watu wengi kujua, kitu kingine wasichokijua ni kwamba mwanaume aliyemuoa anamzidi umri kwa kiasi kikubwa sana.

Hata hivyo mwanakheri alitafutwa na global kuulizwa juu ya swala hilo ndipo aliposema kuwa aliamua kufunga ndoa harakaharaka kwa sababu mume wake alikuwa na safari ya ghafla, na kuhusu swala la mwanaume kuwa na familia Mwanakheri anasema kuwa anachojua yeye ni kuwa mume wake ana watoto tu basi na swala la kuzidiwa umri yeye haangalii ilo anachoangalia ni ndoa yenye staa tu basihayo mengine hawezi kuyasemea.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.