Mwarabu Fighter Afunguka Sababu ya Kufukuzwa kazi WCB

Aliyekuwa mlinzi (Bodygurd) wa msanii na boss wa lebo ya muziki Tanzania WCB Wasafi Diamond Platinumz anayejulikana kwa jina la Mwarabu Fighter afunguka mengi kuhusiana na hatma yake kufanya kazi tena na Diamond.

Mwarabu alifunguka baada ya kupiga stori na Bongo Five,baada ya kukutana nae maeneo ya Samaki samaki mahali ambapo Diamond pamoja na timu yao nzima ya WCB walikuwa na tafrija ya Rom Jones inayohusu birthday yake.

Mwarabu alifunguka mengi sana na hasa baada ya kuulizwa kuhusu kurudi tena kufanya kazi WCB.

Mwarabu Fighter inasemekana alifukuzwa na boss wake Diamond Platinumz kwa kile kinachosemekana kuwa aliwahi kutoka kimapenzi na mpenzi wake Harmonize Sara

Mwarabu Fighter Akiri Kutelekezwa na WCB

Aliyewahi kuwa body guard wa msanii Diamond platinumz na wasanii wake kutoka WCB amefunguka na kusema kuwa tangubalipopata ajali na kuumia vibaya hakuna msanii yoyote  wa WCB aliytaka kumjulia hali wala kumpa pole lakini pengine wana jipanga kwanza.

Hata hivyo Mwarabu Fighter anasema kuwa hata pesa za matibabu na vitu vyote amekuwa akigharamia yeye mwenyewe huko akikiri kuwa ameachishwa kazi sasa ni miezi minne.Hata hivyo alioulizwa kuhusu kutelekezwa, Mwarabu Fighter alijibu kuwa neno la kutelekezwa ni kubwa sasa.

labda linaweza kuwa neno kali sana kusema nimetelekezwa, lakini ukweli ni kwamba sijapata huduma zozote kutoka kwa WCB,pengine wanajipanga kunisaidia sijui lakini kwa sasa ninahangaika na afya yangu mimi mwenyewe, ninashukuru ninaendelea vizuri na nina imani nitapona

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.