Niko Kwenye Mahusiano Tena Yenye Furaha Kabisa ;-Mwasity

Mwanadada Mwasiti amefunguka na kutangaza kuwa kwa umri wake mpaka sasa kusema kuwa  hayupo katika mahusiano ni uongo kwa sababu sio kweli hata kidogo, Mwasiti aliamua kufunguka na kusema kuwa yeye kwa sasa yuko katika mahusiano yenye amani na furaha kabisa.

mwasiti anasema kuwa ni aibu kubwa katka umri wake kusema kuwa hana mahusinao kwa sababu kusema hivyo ni kumaanisha kuwa hafatwi hata na mtu mmoja wakati kiuhalisia iyo so kweli.

Akiongea na FNL, na Sam misago, Mwasiti anasema kuwa “niko kwenye mahusiano, mahusiano yenye furaha kabisa,  na ni mazuri tu kwakweli na kwa umri niliofikia kwenda katika interviews kila siku na kusema kuwa mimi niko single ni aibu kubwa sana.

Watu wengine wamekuwa wakikataa kusema kuhusu mahusiano yao hadharani . lakini mwasiti anaona kuwa kumtaja  mwanaume wako ni swala la kawaidia tu na wala halina shida yoyote.

Mwasiti Adai Umri Hauwezi Kumkatisha Tamaa Ya Kufanya Muziki

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Mwasiti Almasi amefunguka na kuweka wazi kuwa hawezi akaacha kufanya Muziki kisa eti anahofia umri unakuwa unamtupa mkono.

Mwasiti amefunguka na kudai umri wake hauwezi kuwa kikwazo kwake binafsi kwani anaamini bado ana uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi nzuri ambazo zikavutia mashabiki zake.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa radio, Mwasiti amefunguka:

Sijawahi kukata tamaa na muziki bado nina uwezo wa kufanya. Toka nimeanza muziki naweza kusema nimetimiza asilimia 60 ya malengo yangu. Umri sio tatizo katika kufanya kazi maana hata ukimuangalia Joseph Haule ‘Profesa Jay ni mbunge lakini still anaendelea kupiga kazi”.

Hata nje ya nchi kuna  wasanii wenye umri mkubwa lakini huwasikii wameacha kufanya Muziki, licha ya kuwa kuna umri ukifika huwezi kuonekana kwenye majukwaa ukifabya shoo”.

 

Mwasiti Aamua Kumjibu Linex Kuhusu Wimbo wa Leka Dutigite

Ikiwa ni siku chache zimepita tangu msanii kutoka mkoa wa Kigoma Sunday Linex Mjeda alipofunguka na kusema kuwa asilimia kubwa ya wimbo wa lekadutigite ulitengenezwa na kutayarishwa na yeye, msanii  mwenzake kutoka Kigoma mwanadada Mwasiti Almasi amefunguka na kusema kuwa Linex kwa sasa hapaswi kuzungumzia mambo hayo zaidi ya kukaa na kuangalia jinsi gani ya kufanya kitu kikubwa kuliko  kile.

Aache kuongelea vitu vilivyopita, lekadutigite ilishapita nadhani kwa sasa inabidi tuangalie yale yaliyopo tu kama familia lazima kuangalia kitu gani tena kinaweza kutuongezea manufaa lakini sio nani kaandika mistari mingapi, au mistari mingi , maana hiyo ni zaidi ya miaka minne sasa.-Aliongea mwasiti katika XXL ya Clouds Tv

Wasanii Wa Kike Wengi ni Wasumbufu- Mwasiti

Mwanamuziki wa Bongo fleva Mwasiti amefunguka na kudai kuwa wasanii wenzake wengi wa kike ni wasumbufu na wagumu kufanya nao kazi ndio maana anaamua kufanya kazi na wasanii wa kiume.

Mwasiti amefunguka hayo Kwenye Interview aliyofanya na Enews ya EATV ambapo amedai sababu kubwa ya yeye kupenda kufanya kazi sana na wasanii wa hip hop kuliko wasichana Wenzake ni kuwa wasanii wengi wa kike wasumbufu.

Mwasiti ameendelea kufunguka na kudai kuwa wasichana wamekuwa watu wa kulalamika kwenye Radio lakini Hawaii sawa na ndio maana ameamua kuendelea kufanya kazini na wasanii wa kiume na wiki iliyopita alitoa video yake ya wimbo mpya na Billnas.

Kwanza kabisa mimi napenda hip hop, kusema ukweli ukifanya kazi na wanaume hakuna usumbufu ninavyokwambia mimi nimeshafanya kazi na watoto wa kike ila ni wasumbufu sana alafu wanapenda kwenda kulalamika maredioni”.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.