King kiki Amlilia Oliver Mtukudzi

Moja ya wasanii wakongwe nchi King Kiki amefunguka na kusemakuwa kifo cha msanii mkubwa duniani Oliver mtukudzi kimemgusa sana kwa sababu ni moja kati ya wasanii aliokuwa akiwapenda sana kutokana na kazi zake.

akiongea katika power breakfast, mzee king kiki anasema “nimeshtuka sana baada ya kupata taarifa za kifo chake , lakini pia nimeumia sana kwa sababu nilikuwa na mpenda sana na pia napenda sana muziki wake.”

Oliver mtukudzi , msanii kutoka zimbwabwe alikuwa moja ya wasanii waliojulikana sana na kutokana na kutia sana moyo vijana katika kuinua muziki, lakini kubwa zaidi atakumbukwa kutokana na wimbo wake wa NERIA alioimba na kutumika katika tamthilia ya neria iliyoigizwa zamani sana ikijaribu kutetea haki za wanawake wanaokandamizwa na mila.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.