Msanii Aliyeimba Wimbo wa ‘Tanzania Yetu” Anahitaji Msaada wa Matibabu.

Msanii mkongwe wa miaka ya 90, Mzee  Stephen Hizza ambae aliimba wimbo Tanzania yetu ni nchi ya kupendeza anahitaji msaada wa matibabu anayopatiwa kipindi hiki ambacho yuko hospitali.Inaripotiwa kuwa Mzee Stephen yuko hospitali ya Muhimbili katika wodi ya  Kibasila chumba namba 14 akiwa amelazwa huku ikisemekana kuwa anasumbuliwa na tezi dume.

Mzee Stephen ndie aliyekuwa mtunzi wa wimbo wa kuisifu Tanzania wimbo ambao aliutunga na kuuimba mwaka 1966 miaka mitano tangu Tanzania kupata uhuru ambapo kipindi hicho alikuwa chini ya bendi ya Atomic jazz band iliyokuwepo mkoani Tanga.

Mara ya mwisho Mzee Stephen kusikika ilikuwa ni mwaka 2011 alipohojiwa kipindi Tanzania ilipokuwa ikitimiza miaka 50 ya uhuru.

Watu mbalimbali wameombwa kumsaidia mzee huyo kwa chochote walichonacho na hata kama wanaweza kwenda kwa ajili ya kumuona pia wanaweza kwenda katika hospitali hiyo,

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.