Mzee Yusuf afunguka kuhusu kuoa tena baada ya mke wake kufariki

Alhaj Mzee Yusuf hivi karibuni alimpoteza
mke wake ambaye alikuwa akijifungua mtoto wao. Kifo chake kilibadilisha maisha ya Mzee Yusuf na wanawe lakini wamejifunza kuishi hadi watakopo kutana tena.

Hivi karibuni Mzee Yusuf kwa mara ya kwanza alifunguka kuzungumzia ikiwa anapanga kupata mke mwingine. Hata hivyo Mzee Yusuf akili ambao Gazeti la Risasi kuwa suala hilo ni la Allah na akipata bibi basi ataoa lakini kwa sasa ameamua kupumzika na kutulia.

“Suala la kuoa tena ni la Allah, nitamuomba kama akiamua mimi nioe nitaoa, kama pengine amenipunguzia ili nitulie basi nitatulia maana hili jambo linatakiwa subira kwa kila kitu, hutakiwi kukurupuka, nikikurupuka nitajikuta nashindwa mtihani huu ambao Allah amenipa,”

Mzee Yusuf aeleza watoto wanavyomuulizia marehemu mama yao atarudi lini

Siku kumi zilizopita Mzee Yusuf ambaye alikuwa muimbaji wa nyimbo za Taarabu alimpoteza bibi yake mdogo Chiku Khamis akijifungua mtoto wake wa tatu.

Hata hivyo wanawe ambao ni wadogo bado hawajafahamu kilichotokea kwenye familia yao. Mzee Yusuf amefunguka kusema kuwa sasa hivi watoto hawa wamekuwa wakimuulizia mama yao. Mzee Yusuf aliambia Gazeti la Risasi Mchanganyiko kuwa watoto hao wamekuwa wakimlilia mama yao sana huku wakiuliza alipo.

Aliendelea kusema kuwa alilazimika kuwapeleka kwa ndugu wa mama yao, ili kupunguza machungu yao.

Ninapata taarifa kuwa watoto hawaishi kuuliza alipo mama yao na kila wakikumbuka wanalia, hili ni jaribio kubwa ambalo atalazimika kupigana ili kuhakikisha linaisha salama.

Hata hivyo kwa hivi sasa anataka kuwarudisha nyumbani kwake. Aliendelea kwa kusema,

Nadhani huu muda ambao wamekaa kwa ndugu wa mama zao hao unatosha, hivyo nakwenda kuwachukua ili nikae nao mwenyewe, nianze nao maisha mapya ya bila mama yao kwa sababu nahisi ndiyo faraja yangu kwa sasa. Sijawa na maisha, bado nimechanganyikiwa, hivyo naamini nikienda kuwachukua watakuwa faraja yangu maana nikiwa nao naona niko salama zaidi, watoto wangu nitakaa nao mwenyewe maana mimi ndiye baba yao, watakaa na nani tena kama siyo mimi?

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.