Nahrel Ataka Wasanii na Vyombo vya habari Kutengeneza Mashabiki.

Msanii kutoka katika kundi la Navy kenzo , Nahrel amefunguka na kusema kuwa siri kubwa ya msanii kupata mashabiki ni kama msanii huyo atawatengeneza ashabiki wake ili kukuza muziki wake na pia kupendwa na mashabiki hao.

Nahrel anasema kuwa inabidi ifike sehemu wasanii wajua vitu gani vinatakiwa kupewa kipaumbele katika muziki na sio kila kitu kama kiki na mambo yasiyovutia mashabiki lakini vile vinavyoweza kuwapa amshabiki hamsa ya kupenda muziki.

Nahrel anasema kuwa wasanii , vyombo vya habari na wadau wa muziki hawaongelei mambo muhimu ya muziki kama matamasha au wasanii kutoa album lakini wamekuwa wakiongelea mambo yasiyo ya msingi ambayo kwa sanii ni kiki tu.

Ukubwa wa tukio katika muziki  utengenezwa na msanii au chombo cha habari na ndio shabiki anaweza kuamini zaidi, na shabiki huamini sana kama chombo cha habari kinaweza kuzungumzia, lakini shabiki hawezi kufatilia kitu ambacho hakizungumzwi.

 

Nahrel Kuanza kazi na Akon na Kery Hilson

Nahrel ni mja ya wasanii na watayarishaji wakubwa wa nyimbo nchini na kutokana na ufanyaji kazi nzuri amekuwa akijulikana nchini, Afrika na Duniani kwa ujumla , lakini hivi karibuni Nahrel amesema kuwa kwa sasa amekuwa busy sana kiasi kwamba inabidi anaetaka kufanya nae kazi basi inabidi mtu huyo awee kumshawishi sana.

Basi  ukweli ni kwamba licha ya kufanya ngoma nyingi za wasanii wakubwa barani Afrika akiwemo Mr. Eazi na Patoranking, tayari mkali huyo wa midundo ameshafanya kazi na Akon na Kery Hilson.
Akithibitisha taarifa hizo mzazi mwenzie wa kundi la Navy Kenzo, Aika amesema kuwa tayari Nahreel ameshamaliza kufanya kazi hizo na kinachosubiriwa ni muda tu.
Kuna meneja wetu mmoja nchini Marekani ambaye amejaribu kumfanya Nahreel afanye kazi na Akon.. na Kery Hilson soo! Nahreel soon anafanya nao kazi,“amesema

Lakini pia ulikuwa hujui basi nikujuze, kuwa Nahreel ana mtoto mmoja anaeitwa Gold ambae amezaa na mpenzi wake wa muda mrefu na mwanamuziki mwenzake ambae wameunda kundi linaloitwa NAVY KENZO

Nahrel Ajibu Swala la Kupotea Katika Music Production.

Mtayarishaji wa musiki  kutoka katika kundi la Navy Kenzo wakiwa chini ya The Industry Nahrel amefunguka na kutoa sababu za wazi kabia kuhusu sababu zake za kutofanya Production ya music kwa baadhi ya wasanii kwa sasa pamoja na kwamba wamekuwa wakitengeneza nyimbo zao wenyewe.

Nahrel ambae ni msanii na mtayarishaji pia anasema kuwa amekuwa na kazi nyingi kiasi kwamba amekuwa akishindwa kufanya kazi za watu wengine lakini sio kwamba hafanyi kabisa lakini kama kuna anaetaka kufanya na kazi inabidi atumie nguvukubwa ya ziada kumshawishi ili kuaccha mambo yake na kumfanya yeye kazi.

zamani nilikuwa ninaweka muda mwingi katika production lakini sio sasa,sasa hivi nimepunguza muda kwa sababu nimekuwa na vitu vingi vya kufanya,nimekuwa busy sana lakini kama mtu anataka kufanya kazi ya production ni lazima atumie nguvu kubwa sana kunishawishi ambayo itanifanya nimfanyie kazi yake kwa vibe ili itoke vizuri.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.