“Mimi na Ruby Sio Marafiki” Nandy Atoa Povu Baada ya Ruby Kurudi THT

Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka THT, Nandy ametoa povu zito baada ya msanii mwenzake Ruby kutoka familia moja ya THT kurudi tena kwenye uongozi wake wa zamani.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa kuna mpambano mkali kati ya Ruby na Nandy kwenye kila kitu huku baadhi ya mashabiki wakidai kuwa wanafanana uimbaji wao na hata habari za wao kuwa na bifu kusambaa kila kona.

Hivi karibuni wawili hao walitudi kwenye vichwa vya habari na bifu lao krudi upyaa baada ya kupishana kauli ambapo Ruby apidai alipimzika kufanya mziki kwa muda wa mwaka mzimailo ampishe Nandy afanye mziki wake lakini Nandy alikana taarifa hizo na kudai kuwa sababu pekee iliyomfanya mpaka Ruby kukaa kimya ni nyimbo sake alizotoa kutokuvuma kutokana na ugomvi aliokuwa nao na management yake .

Kwenye Interview aliyofanya na Global Publishers Nandy alimwaga Povu lake kuhusiana na Ruby kurudi kwenye management yake ya zamani:

Labda ningeanza kwa kusema mimi na Ruby sio marafiki kila mtu anakuwa na marafiki zake ila kwa sababu wote tunatoka THT basi tunakuwa kama familia tukikutana tutaongea kuhusu muziki basi itaisha hivyo halafu sababu tu amerudi THT haimaanishi basi ndio niwe naye karibu ili niwafurahishe watu hapana mimi siko hivyo ikitokea Kama tutakuwa na ukaribu basi itakuwa hivyo na kama haitawezekana  basi poa tu”.

Lakini pia Nandy amesema kuwa hana tatizo na kufanya kazi na Ruby kwa kuwa hivi sasa wote wapo THT  endapo tu uongozi wake utaona kama ni vyema kwa biashara.

Bifu la Nandy na Ruby Laibuka Upyaa

Mwanamuziki wa Bongo fleva Nandy, amerudi bifuni tena na msanii mwenzake Ruby.

Wasanii hao warembo wamesemekana kuwa wana bifu kwa muda mrefu sana ingawa kila mmoja kwa wakati wake amekana tuhuma hizo na kudai hawana ugomvi.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kuwa Ruby na Nandy wana bifu kwa sababu ya mwanaume ambaye kila mmoja alikuwa na uhusiano naye.

Baada ya kukaa kimya kwa mwaka mzima Ruby aliuanza mwaka huu kwa kutoa nyimbo yake mpya na kwenye mahojiano aliyofanya na Planet Bongo ya East Africa radio, Ruby alidai kuwa aliamua kukaa kimya kwa mwaka mzima wa 2017 ili kumpisha Nandy ili asifananishwe naye.

Nandy hakufurahishwa na Ruby kusema kuwa alikaa kimya kwa mwaka mzima ili kumpisha yeye, Nandy amemchana Ruby na kumwambia aache kujikosha kwani alitoa nyimbo lakini hazikufanta vizuri tofauti ukiachilia tofauti zake na Ruge, Nandy ameendelea kufunguka:

Hapana siamini kitu kama hicho kwa sababu nakumbuka Ruby ana nyimbo kama tatu kazitoa katika kipindi hicho alitoa nyimbo za singeli mbili na wimbo mmoja unaoitwa ‘walewale’ sasa hapo alikuwa amepumzika ama? ni kitu ambacho sio cha kweli, alafu watu wengi wanajua kwamba Ruby alikuwa amegombana na uongozi wake kwaiyo inavyoelekea nyimbo zake hazikufanya vizuri kwa sababu ya ugomvi wake na uongozi wake sasa alinitumia mimi kama kisingizio chake”.

Ruby aliweka wazi kuwa hana bifu na Nandy lakini pia kwenye interview aliyofanya aliimba wimbo wa Nandy unaofanya vizuri hivi sasa ‘Kivuruge’ lakini Nandy alipoambiwa aimbe wimbo wa Ruby aligoma kabisa.

Nilikaa Kimya Kumpisha Nandy Ili Nisifananishwe Naye – Ruby

Mwanamuziki wa Bongo fleva ambaye anajulikana kwa kuwa mkali wa vocal Ruby amefunguka na kusema sababu iliyomfanya akae kimya kwa kipindi kirefu ni kumpisha msanii mwenzake Nandy ili asifananishwe naye.

Ruby ambaye alitamba sana na wimbo wake wa ‘Na yule’ alikuwa kimya kwa mwaka 2017 mzima bila kutoa nyimbo zozote hali iliyopelekea mashabiki zake kumkumbuka na hadi wengine kudhani kuwa kaamua kuachana na muziki.

Ruby alikuwa msanii kutoka nyumba ya vipaji THT lakini kutoka huko huko THT kuna msanii mwingine anayeitwa Nandy baada ya Nandy kutoa nyimbo yake na kupata umaarufu mashabiki zao walianza kuwafananisha Nandy na Ruby na kudai kuwa sauti zao zinaendana.

Kwenye interview aliyofanya na Planet Bongo ya East Africa Radio, Ruby amefungukuka na kudai like kitendo cha kufananishwa na Ruby hakikumfurahisha hivyo akaamua kupumzika muziki ili amuachie nafasi msanii mwenzake:

Nilikaa kimya kwa muda mrefu kwa sababu katika kipindi kile kulikuwa kuna kama kushindanishwa fulani na Nandy kwa sababu siku zote mimi najishindanisha mwenyewe na siongei kwa ubaya nampenda Nandy anafanya muziki mzuri lakini niliona tu ngoja nimpe nafasi afanye anachofanya kuwaonyesha watu yeye kama msanii mpya ambaye ndio alikuwa anatoka na kwa kuwa wote tulikuwa wasanii wa THT tulikuwa na ufanani Fulani katika mziki tuliokuwa tunafanya”.

Ruby ameuanza mwaka huu mpya na wimbo wake mpya unaojulikana kama ‘Are you ready’ lakini pia tangu amerudi amepata mapokezi mazuri toka kwa mashabiki zake.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.