Aslay Atoa Siri ya Wimbo Ninogeshe

Mwanamuziki Aslay amefunguka na kusema kuwa wimbo aliimba Nandy wa ninogeshe ambao umefanya vizuri tangu umetoka katika station mbalimbali aliuandika yeye na alitakiwa kuutoa siku nyingi lakini ilibdi apewe Nandy .

Aslay anasema kuwa nandy alikuwa hana wimbo wa kutoa kwa kipindi hicho hivyo ikabidi wimbo uliokuwa tayari ulioandikwa na aslay apewe Nandy kama menejiment iliyokuwa imepanga na kuona kuwa itakuwa sahishi.

ninogeshe ni wimbo ambao nilitakiwa kuuimba nikiwa na nandy , ila kwa sababu nandy hakuwa na wimbo kwa kipindi hicho ilibidi menejiment iamue kupewa nandy aimbe peke yake.

Hata Nandy pia alishawahi kusema katika moja ya mahijiano yake ya nchini Kenya hivi karibuni kuwa wimbo huo uliimbwa na Aslay.

Nandy na Aslay Wamkosha Mama Samia.

Mwisho wa wiki hii wasanii wawili wanaofanya vizuri katika tasnia ya muziki hasa wimbo wao mpya waliorudia wa Subralkheri , Nandy pamoja na Aslay wamepata bahati ya kukutana na Mh. Mama Samia Suluhu, Makamu wa raisi kwa wimbo huo mzuri ambao umemkosha sana mama huyo.

Aslay na nandy waliamua kuurudia wimbo huo ambao uliimbwa miaka mingi ya nyuma kidogo ,ikiwa  hii ni mara ya pili kwa mara ya kwanza uliimbwa na nasra kidogo mwanamuziki wa taarabu.hata hivyo wimbo huo pia umekuwa ukifanya vizuri katika Radio na Tv station mbalimbali na umekuwa ukiombwa na watu kwa mkupuo.

Mama Samia amesema kuwa amefurahishwa sana na wasanii hao kufanya kazi hiyo kwa pamoja na kuifanya vizuri kabisa na amewaomba waendeelee kufanya nyimbo hizo vizuri na kuacha kujiingiza katika makundi mabaya.

Imekuwa ni kama style kwa sasa kwa wasanii wa bongo fleva kurudia nyimbo za wasanii wa zamani , lengo ni kuwakumbusha mashabiki juu ya wasanii wa wazanii lakini pia kuwaburudisha wazee wa zamani.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.