Msanii Nuh Mziwanda amtangaza kuwa single mpaka sasa hivi tangu alipoachana na mwanamke aliyefunga nae ndoa na kumpatia mtoto Nawal.Nuh maekanusha tetesi za kuwa yeye na Nawali wamerudiana na kusema kuwa wamebaki na jukumu moja tu la kulea mtoto kwa sababu yeye ni baba na anamajukumu yote ya kumlea mtoto wake.
Hapana sio kweli, hakuna ukweli wowote juu ya hilo, tumebaki tu kulea mtoto kwa sababu kama mimi inabidi nisimame kama mwanaume na kuchukua majukumu yangu ili mtoto aweze kupata malezi bora lakini yeye ana mitikasi yake na mimi nina mitikasi yangu.hatupo inlove.
Hapana bado sijaamua kuwa na mwanake bado, mimi niko single, sijafikiriabado kuwa na mwanamke kwa sasa.
Shiloleh ni mke wa mtu na mimi nina heshimu sana mke wa mtu na ndoa ya watu, sio kweli kuwa ninaingilia mapenzi ya watu.
Tangu nuh kuachana na nawal mwanamke ambae aliweza kuza nae mtoto mmoja wa kiume hajawahi kuonekana wala kuvuja kwa tetesi kwa yupo katika mahusiano tena kwa sababu kwa wasanii huwa ni vigumu kutunza siri za kuwa wapo katika mahusiano.hata hivyo siku kadhaa kabla ya ndoa ya aliyekuwa mwanamke wake , zilivuja tetesi kuwa Shilole na Nuh bado wana mapezni ya kisirisiri.