Mwili wa Pancho Waagwa Lugalo Tayari Kwenda Gairo.

MASTAA, wadau wa sanaa ya muziki na waombolezaji mbalimbali wamejitokeza leo Ijumaa, Oktoba 12, 2018, kuaga mwili wa aliyekuwa Producer wa Studio za H-Bits, Pancho Latino, katika Hospitali ya Lugalo jijini Dar.

Pancho maarufu kama Mafia, alifariki dunia juzi jioni kwenye ajali ya kuzama na maji wakati akiogelea kwenye Kisiwa cha Mbudya jijini Dar es Salaam.

Mwili wa marehemu umeagwa leo Dar na katika ibada maalum ya kuaga na utasafirishwa kwenda nyumbani kwao Gairo, mkoani Morogoro kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho Jumamosi, kama ilivyotangazwanhapo awali na baba wa marehemu .

Pancho anasemwa kama moja ya watayarishaji bora wa muziki nchini Tanzania , hivyo tasnia imepoteza mtu bora na muhimu sana.

Pancho Kuzikwa Gairo Mkoani Morogoro.

Baba mzazi wa marehemu Pancho Latino amefunguka na kutangaza rasmi kuwa mtoto wake atazikwa katika kijiji chao kilichopo Gairo mkoani Morogoro .

Baba wa Pancho Latino anasema kuwa amesikitishwa sana na kifo cha mtoto wake ukizingatia kuwa aliweza kuongea nae hivi karibuni kbala ya kifo chake na hata alipoona katika mitandao kuhusu kifo chake alishangazwa sana na taarifa hizo.

Akielezea kwa undani kuhusu taarifa ya kifo hicho, baba wa marehemu anasema kuwa alianza kuona taarifa hizo katika mitandao na kisha kumpigia simu kaka yake aliyekuwa anakaa nae jijini Dar na ndipo alipothibitisha taarifa hizo.

Hata hivyo baba wa pancho ambae ni mchungaji wa kanisa moja mkoani hapo anasema kuwa mtoto wakeatazikwa siku ya jumamosi kama ratiba ilivyo na kama kuna mabadiliko yoyote pia watataoa taarifa zaidi.

Wasanii Wamlilia Pancho Latino, Kifo Chake Chastua Wengi.

Baada ya kusamba kwa taarifa za ghafla za kifo cha moja ya wadau katika sanaa, habari ambazo zimeshtua wengi sana katika tansian hiyo.Wadau mbalimbali wa sanaa na burudani wamejikuta katika wakati mgumuwa kushindwa kuzuia hisa zao na kuanza kutoa pole lakini pia kusambaza habar hiuzo kwa wengine.

Msiba huu mzito wa  producer Pancho Latino uliotokea leo October 9,2018 katika kisiwa cha Mbudya Dar es Salaam.Hawa ndio baadhi ya mastaa walioguswa na taarifa hizo na kuziandika kupitia kurasa zao za instagram

“Pancho Pancho Pancho nimeumia sana sina mfano wa maumivu niliyopata dah! Pumzika kwa Amani na Asante kwa mchango wako mkubwa katika Muziki Wetu…Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe” -Joh Makini

Daaah!!! Upumzike kwa Amani, sidhani kama ulikuwa umemaliza ulichokuwa nacho kichwani. Mapema sana, ila kazi ya Mungu haina makosa #RIP“-Marcochali

“Kutokana na msiba uliotufika hivi punde wa kuondokewa na producer Genius PANCHO LATINO kutoka B’HITS…Hatutaweza kuachia VIDEO Yetu ya#USHINDITENA kwa Leo…SO SAD Kwa kweli R.I.P PANCHO LATINO #RIP#genius#mafia #weusii“-Lordeyesmweus

“Eh Mungu … ? Rest Easy Young Legend. Thankyou for everything you taught me, you raised me #BHitz you will live forever in the music ??. Poleni Sana kwa familia nzima ya #BHitz #LatinoMafia@hermyb pigo kubwa kwenye tasnia ya muziki.” -Vanessa Mdee

“Rest In Power Latino Mafia!!!! ? I am Sad!! -Bdozen

“Doh..Upumzike kwa amani @pancholatino ..kazi ya Mungu na safari yetu ni moja..nimesikitika mno” -Mwana FA

Tanzia: Producer Pancho Latino Afariki Dunia

Mtayarushaji wa muziki wa Bongo fleva kuyoka B Hits maarufu kama Pancho Latino Amefariki dunia kwa ajali ya kuzama majibu wakati anaogelea katika visiwa vya Mbudya.

Taarifa za awali zimedai Pancho alikuwa anaogelea katika fukwe za visiwa vya Mbudya aliingia Kwenye maji kwa nia ya kuogelea lakini kwa Bahati mbaya alizama na mpaka kuja kiokolewa hali yake ilikuwa tayari mbaya na kuwahishwa hospitali ambapo aliaga dunia.

Wadau mbalimbali wa sanaa na burudani wameanza kutoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu mzito.

Bwana ametoa Bwana Ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe, Amina.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.