Petit Man Afunguka Kuhusu Kufumaniwa na Malkia Kareen

kumekuwa na picha zimekuwa zikisambaa zikimuonyesha Malkia Kareen akiwa kituoni na pia upande mwingne zikimuonyesha Petit Man pia akiwa kituo cha polisi , huku akiwa karibu na mmoja wa wanaume alieonekana amevaa dela .

Kwa habari zilizokuwa zikisambaa ni kwamba Petit man amekuwa na mahusiano na Karen kwa muda mrefu na  wikiend hii Petit alimfumania mwanadada huyo na mwanaume mwingine hivyo kuanza kupigana mpaka kumtoa ngeu karee an kesi kufika polisi.

Je kuna ukweli wowote, ukweli unabaki kukwa waili hao wamekanusha tetesi hizo huku petit akisema kuwa matukio yale kweli ni ktuo cha polisi lakini kila mmoja kwa wakati wake, akiandika katika ukurasa wake petit amejilezea kama inavyoonekan.

Petit Alikataa Kuwa Muoaji Kwenye video Yangu :-Karen

Mwanadada karen amefunguka na kupangua tetesi za kutembea na Petit man kama ambavyo katika mitandao ya kijamii wamekuwa wakisema na pia mke wa awali wa Petit kusema kuwa anavyojua yeye ni kuwa mwanadada karenamekuwa akiishi kinyumba na Petit kwa muda sasa.

Karen anasema kuwa yeye na petit walikuwa marafiki na wataendelea kuwa marafiki na hata katika video ya washa Petit alikataa kata kta akuwa bwana harusi  na kwamba ilichukua muda mrefu sana mpaka kumfanya akubali swala hilo.

Akielezea kwa kirefu zaidi, Karen anasema kuwa walipokuwa wakirekodi weimbo huo studio Petit alikuwepo kwa shughuli zake na alipousikia wimbo alisema kwa utani kuwa huo wimbo inabidi kuwe na bwana harusi na kusema kuwa yeye atakuwa lakini kumbe hakuwa serious na swala hilo.

Hivyo basi hata baada ya maandalizi ya shooting kuisha walijikutwa wakimtegemea petit kama bwana harusi kitu ambacho kiliwafanya kumtafuta na alikataa akasema kuwa alikuwa akitania wala hawezi kufanya hivyo.

Karen anasema kuwa ilichukua muda na nguvu kumshawishi akubali na hata alipokubali  hakutaka kutangaza kwa kila mtu kuhusu ilo na hata picha zilivyovuja alitumia nguvu kuelezea watu wake wa karibu na ndugu zake pia.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.