Mke Wa Pfunk Agoma Kumuacha Kajala Awe Mama Mwenye Nyumba

Mke wa Prodyuza maarufu na mkongwe kwenye mziki wa Bongo fleva P Funk majani, Samira ameibuka na kudai atapambana na Kajala na kamwe hatamuachia nyumba.

Kwa Miezi kadhaa Kumekuwa na tetesi kuwa PFunk na Ex wake ambaye pia mama watoto wake aliyezaa naye mtoto mmoja Kajala wamerudiana kitu kinachomuweka Pabaya mke wa Pfunk ambaye hivi sasa ni mjamzito.

Samira ambaye wiki iliyopita ilisemekana alikuwa tayari kumuacha Pfunk na kurudi kwa wazazi wake Arusha, inadaiwa ameamua kupambana na Kajala na kukataa kumuacha Kajala amchukue mumewe.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Samira ameongea kwa uchungu huku akidai kila siku huwa anaumizwa pale anapokutana na kashfa kumuhusu mume wake na Kajala lakini ameamua kubaaki kupambana.

Yaani mateso ninayokutana nayo kwenye ndoa yangu ni Mungu pekee ndio anajua tena kwenye hali hii ya ujauzito niliyo nayo, awali nilipanga niondoke nimuachie nyumba lakini nimeona nikomae hadi kieleweke“.

Mara nyingi Kajala alipokuwa akiulizwa kuhusiana na kuingilia ndoa hii ya mzazi mwenzie amekuwa akikana mara na kusema kuwa kuwa P Funk ni baba wa mtoto wake na si vinginevyo ingawa video mbalimbali zinavuja zikiashiria ni wapenzi.

Video Ya Kajala na Pfunk Yazua Utata Mtandaoni

Muigizaji wa Bongo movie Kajala Masanja na mtayarishaji wa Muziki Pfunk Majani wamerudi Kwenye headlines na tetesi za kurudiana baada ya kuposti video zenye utata mtandaoni.

Kwa wiki kadhaa sasa kumekuwa na tetesi mbali mbali zinazodai kuwa Kajala na mzazi mwenzake Pfunk ambao wamezaa pamoja mtoto mmoja wamerudiana na Pfunk kumuacha mke wake ambaye ni mjamzito kwa ajili ya Kajala.

Mara kadhaa Kajala na Pfunk walikataa taarifa hizo lakini siku ya jana video iliwaonyesha wakibusiana iisambaa mtandaoni na mara moja tetesi za wawili hao kurudiana zilishika kasi.

Kwenye video hiyo inayowaonyesha Kajala, Pfunk pamoja na mtoto wao Paula wakiwa kwenye gari huu wakifurahi ndipo Pfunk alipoinuka na kumbusu Kajala shavuni:

 

Mpaka sasa wawili hao hawajathibitisha taarifa za wao kurudiana ingawa ingawa mke was Pfunk aliwatuhumu kwa kurudiana siku chache zilizopita.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.