Kifo Cha Masogange Kimenifunza Mambo Mengi- Preety Kind

Video vixen aliyegeukia sanaa ya Bongo fleva Suzan Michael ‘Preety Kind’ amefunguka na kudai Kifo Cha msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ kimemfunza mambo mengi.

Preety Kind ameweka wazi kutokana na kifo hiko kimemfanya aendelee kubadili mwenendo wake wa maisha kwani huwezi kujua siku wala saa ambayo unaweza kufa.

kwenye mahojiano na Za Motomoto News, Pretty Kind alisema kifo hicho kimempa funzo kwani hapishani sana umri na Masogange hivyo kimemwaminisha kwamba kufa kunakuja wakati wowote haijalishi una umri mkubwa au mdogo kwa hiyo amejikuta akizidi kubadilika na kuachana na maisha ya starehe yasiyompendeza Mungu.

Kifo cha Masogange kimeniumiza sana mpaka niliugua ghafla na kushindwa hata kwenda kuuaga mwili wake pia kimenipa funzo kubwa maana maisha aliyokuwa anaishi ndiyo nilikuwa naishi mimi zamani kabla sijaanza kubadilika, nilikuwa naishi maisha yasiyompendeza Mungu, kujiachia kwa sana lakini kwa sasa nimezidi kubadilika kutokana na kifo hiki muda mwingi natumia kumuomba Mungu na kufanya kazi kwa bidii maana kifo kipo wakati wowote”.

Preety Kind alifungiwa kujihusisha na sanaa Miezi michache iliyopita baada ya kudaiwa kuvaa nusu uchi lakini amedai alianza kubadilisha mwenendo wake na hivi sasa yupo vizuri.

Preety Kind: Naomba Waziri Anipunguzie Adhabu Maisha Magumu

Mwanamuziki wa Bongo fleva na Muigizaji, Preety Kind amefunguka baada ya kimya kirefu na kuiomba serikali msamaha na kumuangukia Naibu Waziri Juliana Shonza amsamehe.

Preety Kind aliyekuwa anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘vidudu washa’ aliomshirikisha Gigy Money alifungiwa mapema mwaka huu kwenye kufanya kazi zozote za kisanaa baada ya kutuhumiwa kuvaa nusu uchi mtandaoni na hata nyimbo yake kukosa maadili.

Waziri Juliana Shonza alitangaza kuwa Preety Kind atafungiwa kwa muda wa miezi Sita ambapo hatakiwi kujihusisha na kazi zozote za kisanaa huku pia akaunti yake ya Instagram aliyokuwa anarusha picha zake za nusu utupu kufungwa.

Ikiwa Miezi michache imepita yangu adhabu hiyo itangazwe Preety Kind ameibuka na kula kama kuwa maisha kwake yamekuwa magumu kwani sanaa ndio ilikuwa njia yake pekee ya kuingiza kipato kwenye maisha yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Preety Kind amefunguka na kusema kuwa kwa sasa yupo kwenye harakati za kumuandikia Waziri Juliana Shonza barua ya kuomba apunguziwe adhabu kwani Mambo yanamuendea kando.

Nimeshaomba sana msamaha na ninaendelea kuomba ambapo kwa sasa ninaandika barua ya kuomba msamaha kwa Naibu Waziri maana maisha yangu hayaendi ni magumu”.

 

“Sijahongwa Elfu 20 Kisa Nimefulia Wanaume Wengi Bado Wananisumbua”- Preety Kind

Msanii wa Bongo fleva Susan Michael maarufu kama Preety Kind amefunguka na kudai kuwa habari za yeye kufulia hadi kuhongwa elfu ishirini sio za kweli kabisa ni uzushi tu.

Msanii huyo alipata umaarufu kwa mara ya kwanza mtandaoni kwa vituko vyake na kupenda kukaa uchi lakini baadae alikuja kujiingiza kwenye kuigiza filamu za bongo movie lakini pia alidai haina soko na hivyo kupelekea kuingia kwenye kuimba Bongo fleva ambapo mara ya mwisho alikuwa anatamba na wimbo wake aliomshirikisha Gigy Money unaoitwa ‘Viduduwasha’.

Lakini wiki chache zilizopita Pretty kind alifungiwa na BASATA kujihusisha na shughuli zozote za kisanaa kwa muda wa miezi sita. Tangu amefungiwa kumekuwa na maneno maneno mtandaoni huku wengi wakidai kuwa anahongwa shilingi elfu ishirini na wanaume maneno aliyokataa.

Kwenye mahojiano na Millard Ayo TV Pretty Kind amezidi kufunguka yafuatayo:

Kwanza nikirudi kwenye sanaa nataka nifanye au niimbe nyimbo ambazo zitawaonyesha watu kuwa kweli Pretty Kind kabadilika alafu pia nataka niwahakikishie watu hizi stori za mimi kuishi kwa kutegemea kuhongwa sio za kweli kabisa eti kwenye mitandao wamesambaza habari kuwa nategemea kuhongwa shilingi elfu ishirini sio kweli kabisaa na wale wanaume wanaoniona ninashida wanataka wanusaidie nawaambia kabisaa wasinisumbue maana sahivi nasumbuliwa sana na wanaume”.

Lakini pia Pretty kind amedai kuwa kwa kipindi hiki ambacho amekuwa kimya ameshajifunza sana na amebadilika tofauti na alivyokuwa mwanzoni kipindi cha nyumba hivyo hata akimaliza hiyo miezi sita hategemei kurudi Kyle alikotoka.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.