Reginald Mengi Afunguka Jinsi Jacqueline Alivyookoa Maisha Yake

Mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya IPP Reginald Mengi amefunguka jinsi mke wake  aliyewahi kuwa Miss Tanzania Mwaka 2000 Jacqueline Ntuyabaliwe alivyookoa maisha yake.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kituo cha Televisheni cha Citizen cha Kenya, Mzee Mengi amefungukia mahusiano yake na Jacqueline Mengi na kudai kinyume na watu wanavyofikiria haikuwa rahisi kwake kumpata mlimbwende huyo:

Niliwahi kumsikia lakini hatukuwahi kuonana lakini ikatokea nafasi wakati nipo safarini Uingereza ambako nilikuwa na shughuli za kibiashara na Jacqueline alikuwa yuko jijini Birmingham kwenye shughuli zake za muziki”.

Nilitaka kuonana naye wakati yupo Uingereza kwa hiyo nikimualika kuja London kutoka Birmingham huwezi amini hakuja! Lakini nikiendelea kuwasiliana naye kwa simu mara kwa mara lakini hatukukutana lakini tuliporudi Tanzania nilimfukuzia Mpaka alipokubali kwenda matembezi na mimi”.

Mengi amefunguka kuwa baada ya ndoa na kupata watoto mapacha na Mlimbwende huyo, Mengi mwenye miaka 75 anasema kwamba asingekuwa na mrembo huyo labda angekuwa ameshafariki.

Lakini pia Kupitia kitabu chake kinachoelezea maisha yake ‘I can I must I will’ Mengi anazungumzia mrembo huyo Kama mtu aliyeleta mwangaza katika maisha yake.

 

“Wewe Ndio Hewa Ninayopumua” Reginald Mengi Kwa Mkewe Jacqueline

Mfanyabiashara Bilionea na Mkurugenzi wa IPP Media, Reginald Mengi amefunguka mazito kwa mkewe mrembo Jacqueline Mengi siku ya Jana iliyokuwa siku yake ya kuzaliwa.

Uhusiano kati ya Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi ambaye alikuwa Miss Tanzania miaka ya nyuma na  Mzee Mengi ulizua gumzo sana kutokana na tofauti kubwa iliyopo kwenye umri wao kwani Mengi ana watoto wakubwa zaidi ya Jacqueline na kwa upande wa Jacqueline Mengi anafaa kabisa kuwa baba take hivyo habari za uhusiano wao zilishtua wengi.

Lakini usemi unaosema ‘Umri ni namba tu’ ulizidi kudhihirika pale ambapo Mengi na Jacqueline walizaa watoto wao mapacha wa kiume na hatimaye miaka miwili iliyopita walifunga ndoa katika visiwa vya Seychelles.

Siku ya Jana ilikuwa birthday au sherehe ya siku ya kuzaliwa ya bibie Jacqueline na mumewe Mzee. Mengi hakusita kumpa yaliyo moyoni mwake kwani kwenye ujumbe wake aliouweka kwenye mtandao wa Twitter alifunguka kuhusiana na mapenzi yake mazito aliyonayo juu ya Mkewe hadi kufikia hatua ya kumjulisha kuwa bila yeye kuwepo maishani mwake hataweza kuishi kwa sababu yeye ndio pumzi take.

Happy birthday My Love, I wish many more happy years full of fun, happiness and love Jacqueline you are the air that I breath”.

Hizi ni baadhi ya picha zinazomuonyesha Reginald Mengi na Jacqueline lakini pamoja na watoto wao.:

 

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.