Madee Akosoa Uvaaji wa Roma,Hana Muonekano wa Msanii.

Msanii wa muziki nchini ambae anafanya vizuri na wimbo wake wa sema Madee  amefunguka na kusema kuwa mwanamuziki mwenzake Roma hajui kuvaa na hana hata muonekano wa kisanii kama wasanii wengine.Madee amesema hayo alipokuwa akiongea na Clouds Tv na kusema kuwa roma inabidi abadilishe namna ya uvaaji ili apate muonekano wa kisanii maana hajui kuvaa.

Kati ya wasanii wa bongo ambao wananiangusha sana katika uvaaji ni roma na nilishamwambia na kufikiria kuwa siku moja inabidi nimpeleke  dukani nikafanye nae shopping kwanza  kwa maana jinsi anavyovaa uwezi kusema ni msanii.

Madee amekuwa akiwakosoa sana wasanii kuhusu kuvaa huku akimpa kiburi msanii wake wa tip-top kwa Dogo Janja kuwa ndie msanii peke bongo anaejua kuvaa kuliko wasanii wengine.Roma na Madee ni wasanii wa muda mrefu na wamekuwa wakijibizana kiutani kwa muda mrefu na hata wakati mwingine kufikiriwa kuwa inawezekana wawili hao waka wa na bifu lakini sio kweli.

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.