Roma Sio Mchizi Wangu:-Moni Centrozone.

Msanii wa bongo fleva Moni Centrozone amefunguka kna kumkana msanii mwenzake roma na kusema kuwa wala sio mchizi wake na wala hamjui na hajui nyimbo zake zozote na amekuwa hamfatilii kwa chochote kile,

Moni na Roma walikuwa wasanii waliokuwa wakifanya kazi pamoja na hata walipopata matatzio ya kutekwa na watu wasiojulikana walikuwa wote na kupitia matezo  waote lakini baada ya kumaliza matatizo hayo wawili hao walianza kuonekana hawafanyi kazi pamoja na kila mmoja kuonekana kutojali anachafanua mwenzie.

Hata hivyo alipowahi kuulizwa Moni alikiri na kusema kuwa kilimkera sana kitendo cha Roma kuchukua nafasi kubwa sana katika vyombo vya habari baada ya wao kutekwa kana kwamba wao hawakukumbwa na matatizo hayo.

Alipokuwa akiulizwa kama ameusikia wimbo mpya wa roma na stamina Moni alijibu “Roma sio mchizi wangu, wimbo wake siujiu na wala sina muda wa kuijua.”

MONI Azidi Kumpondea Roma ,Asema Anaweza Lolote Bila Yeye.

Ukaribu wao kipindi cha kwanza kuliwafanya mashabiki wa hip-hop kuzidi kupenda mzuki wao kwa sababu muda mwingi walikuwa wakionekana kuwa pamoja na kufanya kazi pamoja kwa sababu tu walikuwa ni marafiki ambao walikuja kuwa kama familia.

Hata hivyo baada ya wasanii hao wawili Moni na Roma kupata jnaga la kutekwa na baadae kurudi uraiani ndipo ilipoanza kuonekana kama watu hawa wanatofauti ambazo wameshindwa kuzimaliza na kufikia hatua ya kwagawa hata mashabiki.

Moni alishawahi kuweka waiz kuwa kitu kikubwa kilichomfanya hashindwe kuelewana na Roma ni baada ya kutekwa ambapo Roma aliamua kutunga wimbo wake peke yake kana kwamba janga hilo lilimpata peke yake na hata katika mahojiano na vyombo vya habari yeye ndio alikuwa kinara kuliongelea swala hilo kuliko wengine.

mwandishi wa GPL, aliamua kumtafuta Moni ili kujibu tuhuma hizo za kugombana na rafiki yake na aliyekuwa msanii mwenzie na kufanya kazi pamoja huku mada kubwa ikiwa ni kwamba Moni aliamua kuunda kundi lake na Country Boy ili kushindana kimuziki na Roma ambae ameunda kundi na Stamina.

sio kweli kuwa nimeunda kundi la kimuziki kwa ajili ya tofauti zetu na roma,na hata swala la watu kuungana na kufanya kazi hayo yameanza zamani sana.roma na stamina sio wa kwanza kuna kina chrgge na temba walifanya kazi pamoja hata mwana afa na ay pia.

na kila kitu kina wakati wake sikuungana na roma huko nyuma  kwa sababu hata counrty ni mtu wangu wa zamani sana kwa sababu alikuwa akinisapoti sana kipindi cha shoo zangu kwaio niliona tukiungana tunaweza kufanya kazi.

Akielezea sababu ya kutengana na Roma, Moni anasema kuwa roma alianza kumuacha katika kazi zake wakati muda mwingi walikuwa wanatakiwa kufanya kazi pamoja.

ni kweli mimi na Roma kuna vitu vingi tumefanya katika muziki,na sikatai kuwa yeye ndio alikuwa akinipokea Tongwe Records, na kupitia yeye niliweza kujuana na watu wengi lakini niliona kabisa ilifika muda mimi nilianza kuwa kikwazo katika shughuli zake,hivyo vitu vingi akaanza kuvifanya peke yake na kuniacha nyuma kwaio mnapofika stand alafu mkalala na ukiamka asubui unagundua mwenzako alitaka kukuacha basi ni lazim  uangalie kitu.

Hata hivyo Moni laisema kuwa pamoja na hayo yote kutokea lakini hawezi tena kukaaa chini na Roma wakayazungumza kwa sababu tayari anaweza kufanya kila kitu mwenyewe.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.