BASATA Wakanusha kuifungia Parapanda.

Katika ukurasa wake wa Twitter Roma Mkatoliki aliandika wiki iliyopita na kusema baraza la sanaa tanzania linaua vipaji na muziki wa tanzania kwa kile wanachokuwa wakikifanya , hii ni post iliyoandika na roma ikiwa ni kama siku tatu tu tangu walipotoa wimbo wao uliokwenda kwa jina la Parapanda.

Hata hivyo baada ya hapo wikiendi yote iliyopita , habari ziliozkuwepo katika mitandao ya kijamii na vyomba vya habari ni kwamba wimbo wa parapanda umefungiwa na BASATA , huku ikisemakana kuwa wasanii hao waliitwa kuhojiwa kuhusu wimbo wao.

Sasa basi , BASATA wamefunguka na kuongelea trending news ya parapanda na kusema kuwa habari zinazosambaa kuwa wasnaii hao wameitwa basata sio kweli na hakuna kitu kama hicho labda wawe wanatafura kiki.

BASATA wansema kuwa waanii hao watakuwa wameamua kujifungia wimbo huo kwa nia ya kutafuta kiki na kuuza wimbo huo lakini wao kama baraza hawajawaita wasanii ROMA  na STAMINA kama ilivyokuwa imeripotiwa.

Stamina Atoa Dukuduku Lake Kuhusu Wimbo wa Kibamia na Kufungiwa kwa Roma.

Msanii mwenzake na Roma ambae kwa pamoja  wanaunda kundi la ROSTAM , Stamina amefunguka na kuongea kwa uchungu kuhusu kufungiwa kwa wimbo wao wa kibamia na msanii mwenzake kukatazwa kufanya kazi kwa muda wa  miezi sita na kusema kuwa Baraza la Sanaa Tanzania linafanya kwa ajili ya kuwakomoa na sio kuwarekebisha kama wenyewe wanavyosema.

Stamina ansema kuwa kwa muda ambao Baraza la Sanaa waliwapa wasanii hao kwa ajili ya kufanya marekebisho ya wimbo huo bado haujafika lakini cha kushangaza ni kwamba wimbo na msanii vyote vimefungiwa wakati mara ya kwanza walipoongea na naibu waziri huyo walipewa miezi sita

Kibamia imetoka  novemba 22,017 na BASATA na Roma mkatoliki tuliitwa desemba 6 2017 na mh waziri  akasema kuwa anatupa miezi miezi sita kufanya marekebisho lakini leo ndio kwanza march 1,2018 mbona hata miezi sita  bado au miezi sita ya tanzania iko tofauti na kalenda za duniani.mna tatizo gani na wasanii wetu  BASATA na wizara, mnakuza  au mnaua sanaa?.

Swala la kufungiwa kwa msanii roma kumezua maneno mengi sana katika mitandao huku wengi wao wakisema kuw kitendo cha kuufungia wimbo ilikuwa ni adhabu tosha kwa msanii huyo kwa sababu ni kazi mabayo ndio inamlishia familia yake.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.