“Nilikuwa nakunywa pombe sana” Saida Karoli

Kama wasanii wengi Saida Karoli ambaye ni muimbaji na pia mama hivi karibuni alifunguka kueleza baadhi ya vitu ambazo zilimfanya kuteleza kutoka kwa muziki akizungumza kwenye mahojiano na Clouds FM.

Saida ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya wa ‘Orugambo’, alisema kuwa alijipata ameanza kutumia pombe lakini baada ya kugundua kuwa haikuwa na faida basi aliwacha na tangu 2006 hajagusa ata bia… Saida alisema,

“Vitu vingi nilipitia ila namshukuru Mwenyenzi Mungu sikufikia hatua ya kusema najiuza, na mpaka mtu anafikia anaona yeye sio kitu anaenda kujiuza barabarani, kuuza mwili wake lakini mimi sikufanya hivyo,”

Msanii huyu aliendelea kusema,

“Nilikuwa nakunywa pombe sana lakini kutokana na kushuka kwangu nikaona na pombe niache tangu mwaka 2006, situmii bia, situmii Sigara namshukuru Mwenyenzi Mungu amenipa ustahimilivu nimesimama wima hatimae nimerudi Saida yule yule.”

Hata hivyo kwa sasa amejiandaa kuwachia album yake hivi karibuni.

 

Saida Karoli afunguka kuhusu kazi yake na Diamond Platnumz

Muimbaji mkongwe Saida Karoli amefunguka kukiri kuwa ameweza kufanya vizuri na wimbo wake mpya, Urugambo.

Hata hivyo aliendelea kusema kuwa katika album yake mpya amemshirikisha Bella 9 na Diamond Platnumz. Akizungumza kwenye interview Saida Karoli alisema kuwa hizi projects zake ambazo zitawatoa mashabiki jasho.

“Urugambo nimetoa kama zawadi kwa Watanzania, niliona nijitambulishe kama chai ya asubuhi, lakini watarajie mambo makubwa kwani hivi karibuni mimi na Belle 9 tutatoa kazi ambayo itawatoa jasho mashabiki wa muziki,”

Muimbaji aliendelea kudai kuwa kwa hivi sasa anapanga kuachia nyimbo nyingi kali ili kuwakumbusha mashabiki wake alivyokuwa hapo mbeleni. Pia anapanga nyimbo kufanya vizuri kwa sababu kwa hivi sasa Kuna wasanii wa Kisasa ambao anapaswa kuwafikia kimziki.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.