Sanchi Azungumzia Swala la Kukodi Ndege Yake

BAADA ya kusemekana kukodi ndege binafsi akitokea Dar kuelekea mkoani Iringa, mwanamitindo maarufu Bongo, Jane Rimoy ‘Sanchi’ amefunguka kuwa hajawahi kukodi ndege zaidi ya kupanda kama abiria wengine.

Akizungumza na Za Motomoto, Sanchi alisema kuwa, alipiga picha tu kama wanavyopiga watu wengine wakishuka kwenye ndege, lakini siyo kwamba alikodi na pia bado hajafikia hiyo hadhi ya kukodi.

Siwezi kukodi ndege bana, hiyo ilikuwa na abiria wengi tu na mimi nilikuwa ni mmoja wa abiria ila nilipiga picha wakati watu wameshuka ikaonekana nipo peke yangu,” alisema Sanchi.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.