Sister P Kurudi Tena Kwenye Bongo Fleva

Msanio mkongwe wa muziki wa Bongo fleva aliyewahi kusambaa Kama mmoja wa Wasafi wanaochana miaka ya hiyo Happy Pela ‘Sister P’ ametangaza kurudi tena kwenye gemu.

Sister P ametangaza Kurudishwa kwenye gemu na mwanadada Matata ambaye ameamua kumsimamia ili aonyesha kipaji chake cha kuchana alichokuwa nacho tangu zamani.

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Sister P anayetamba na Ngoma ya Tingisha alisema kuwa, kipaji anacho sana ila alikuwa hana mtu wa kumuinua na kumsimamisha hivyo anamshukuru sana Matata kwa kumfikisha alipo.

Yaani naamini hata upoteeje Mungu anaweza kukuibua kivingine kabisa kama alivyomleta Matata, yaani hapa nilipo niko vizuri kabisa na hata kama nilipotea kwa kukosa muongozo sahihi huyu dada ameniinua vilivyo kabisa“.

Miaka ya nyuma Sister P aliwahi kutamba na ngoma yake inayoitwa ‘Anakuja’ lakini alijizolea umaarufu zaidi Baada ya kuwa na Bifu na msanii mwenzake anayeitwa Zay B.

Sister P-Zamani Muziki Ulikuwa Kazi Sahivi Umekuwa Biashara Tu

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva aliyekuwa anafanya miondoko ya kuchana mwanadada Sister P ameibuka na kudai kuwa sahivi muziki umekuwa biashara na sio kazi kama zamani.

Sister P ameiongelea gemu ya Bongo fleva ilivyobadilika na kutofautiana na zamani ambayo walikuwa wanafanya wao ambapo amedai sasahivi vijana hawaimbi bali wanafanya bishara.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Media Sister P ameendelea kufunguka yafuatayo:

Utofauti upo mkubwa tu kipindi kile sisi tulikuwa tunafanya kazi enzi zile lakini sahivi naona watoto wanafanya biashara Muziki sahivi umekuwa biashara tofauti na kazi, sisi tulikuwa tunfanya kazi tunaingiza kipato sawa lakini sasa biashara imekuwa kubwa sana hawa watoto wanalipua tu.

Unakuta msanii anafanya kazi leo kesho kaitoa studio zimekuwa nyingi wasanii wamekuwa kibao na wengine wanakuwa kama wanazingua hivi tofauti na kipindi chetu ilikuwa kazi mpaka kutoka lakini sahivi mtu anakutupuka anaenda studio anatia voko kesho anaamka na nyimbo imetoka na watu wanaisikiliza”.

Sister P alijizolea umaarufu miaka ya nyuma Kupitia wimbo wake wa ‘Anakuja’ lakini pia kutokana na bifu lake na msanii mwenzake  Mwanadada Zay B.

Sister P Kurudi Mzigoni, Atamani Kufanya Kazi Na Alikiba

Mwanadada mkongwe katika game la muziki wa kizazi kipya sister p, ambae alikuwa kimya kwa kipindi cha muda mrefu ametangaza kuja na ujio mpya huku akitamani sana kufanya kazi na moja ya wasnii wanaofanya vizuri sasa katika soko la muziki alikiba  na anaamini kuwa watafanya kazi nzuri.

Sister P ambae alikuwa akitamba sana kipindi cha nyuma na nyimbo zake kama Anakuja,Hey dj, na nyingine nyingi alizofanya na wasanii wenzie wakubwa  ameongea na studio za East Africa Radio na kusema kuwa anakaribia kuingia sokoni tena kwa kishindo kwa sababu amewamiss mashabiki zake lakini pia anasema kuwa kwa muda mrefu sana amekuwa akitamani kufanya kazi na Ali kiba kwa sababu yeye na Ali Kiba  sio wasanii bali ni wanamuziki hivyo wimbo wao lazima utakuwa mzuri sana.

Kwa sasa nimejipanga vizuri ili kuweza kufanya vizuri mashambulizi ya muziki kwa sababu nina rudi tena katika muziki. Mwakani mwezi wa kwanzakuna ngoma nyingi sana ndani, nimefanya na mtayarishaji mpya katika muziki anaitwa Banny Music chini ya  Big Sound Studio.Lakini kiu yangu kubwa kabisa ni kufanya kazi na msanii Ali kiba kwani naamini kuwa itakuwa kazi nzuri sana na kubwa kwa sabau tutakuwa tumekutana wanamuziki sio wasanii. Alifunguka mwanadada huyo.

Hata hivyo mwanadada huyo ambae alikuwa na muonekano wa kiume hapo awali kwa sasa anarudi kwa kishindo na kusema kuwa  atawashangaza watuw engi kwa sababu ana mpango wa kurudi kitofuati katika muziki na hata muonekano wake pia hautakuwa kama wa mwanzo.Mwanadada huyo anasema kuwa licha ya kukaa kimya kwa  muda mrefu katika game la muziki lakini atakapo rudi bado atajitahidi kurudi katika nafasi yake kwani anaamini kuwa anaweza sana.

Wasanii wengi wa muziki wakongwe wa muziki waliokuwa wamekaa kimya kwa muda mrefu wameanza kurudi katika gam, hii ni kutokana kuwa muzikinwa sasa umekuwa na mafaniko yanayoonekana na umekuwa ni tofauti na ule wa kipindi cha mwanzo.

 

 

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.