Snura- Msambwanda Wangu ni Originali

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Snura Mushi au maarufu kama Mama wa Majanga amefunguka na kuweka wazi kuwa shepu lake alilokuwa nalo ni originali na sio feki kama watu wengi wanavyosema.

Snura ambaye anajulikana kwa kufanya video au shoo ambazo zinakuwa nje ya maadili hasa k a sababu ya uchezaji wake ambao umesababisha kufungiwa baadhi ya nyimbo zake huku hayo yite yakisababishwa na umbo lake.

Kwenye mahojiano na EATV, Shilole amefunguka na kudai hajawahi kutumia dawa za kichina za kuongeza makalio kama watu wanavyomwambia bali umbo lake ni ‘original’.

Nina utofauti kidogo jinsi nilivyoumbwa mimi kiukweli ukiacha hiyo shepu yangu watu wanayoiongelea …Mimi ukiniangalia tu unajua tu ni ‘Original’ kwa sababu kwanza naweza kuongeza kalio kwa kuliongeza lakini je na nilivyokatika ? naweza kuchukua kisu nikajichimba, mimi nilivyo hapa katikati nimetumbukia kabisa yaani nimegawa mgongo pekee yake na chini peke yake“.

 

Snura Aitwa Tena BASATA, Abanwa kwa Masaa Matatu

Mwanadada snura majanga ameitwa tena basata ikiwa hii ni mara ya pili  sasa baada ya kuweka video katika ukurasa wake na video hiyo kusambaa ikimuonyesha akiwa jukwaani akicheza huku ikisemekana kuwa video hiyo haina maadili na haikupaswa kusambazwa.

hata hivyo kikao hicho kilichodumukwa masaa kama matatu , hakijajulikana msanii huyo aliambiwa nini lakini hata aliponwa na waandishi wa habari hakutaka kuzungumzia swala hilo.

Snura Kubadilishwa Mavazi na Mwanaume Wake

Pamoja na kuwepo kwa tetesi nyingi na migongano mingi sana kuhusu penzi jipya la Snura na mwanaume aliyekuwa akisemekana kuwa ni mwanaume wa Nisha, mwanaume huyo anaejulikana kwa jina la Minu amesadikika kumbadilisha namana ya kuvaa mwanadada huyo na kumtaka avae nguo za kumsiti kutokana na umbo lake.

Mwanaume huyo ambae inasemekana kuwa ni mshika dini pia inasemekana kuwa hakuwa anapenda kumuona Snura akivaa nguo zake za kubana au kujiachia sana hivyo amemtaka kuvaa nguo za kujistiri sana na mwili wake kwa sababu anaona kabisa kuwa nguo nyingi akivaa zinakuwa zinatoa ushawishi kwa wanaume.

Akiongea na waandishi wa habari moja ya marafiki wa snura anasema kuwa anaona kuwa minu alikuwa anaogopa kuibiwa hasa kwa sababu ya kuwa mwaamke huyo amekuwa na umbo la kuvutia sana hasa anapovaa nguo za kubana.”jamaa naona amehisi ataibiwa kwaio amemwambia abadilike na abadilishe mavazi.”

Alipopigiwa simu na kuilizwa kuhusu tetesi hizo, snura aliangua kicheko na kusema “hahaaaa nimeamua tu kubadilika mwenyewe.’

Snura Asema Faiza Ally Anatafuta Pa Kutokea

Baada ya kugombana kwa muda mrefu na kutupiana maneno katika mitandao ya kijaamii baada ya msanii Faiza Ally kuweka picha yake iliyoonesha utupu wake akiwa leba kipindi anajifungua mtoto wa pili amabapo watu wengi ikiwepo wasanii kukwazika na kitendo cha mwanadada huyo kudharirisha wanawake wenzie na ndipo Snura alipoamua kumtolea uvivu na kumwambia ukweli.

Hata hivyo baada ya Snura kumwambia ukweli ilileta tafrani kwa sababu Faiza aliona kitu alichokifanya yuko sawa kabisa tofauti na vile watu walivyochukulia.

Mwanadada Snura amefunguka tena na kusema kuwa alichokifanya mwanadada huyo ni kosa la kimaadili kwa jamii sema kuzuka kwa ugomvi wao ni sawa na kutafuta kiki kwa dada huyo kwa sababu nyimbo ambazo yeye anaimba haziweka maungo ya mwili wa mwanamke uchi kama alivyofanya yeye hivyo mwanadada huyo anatafuta pa kutokea tu.

Akiongea na Risasi, Snura anasema kuwa kwanza nyimbo zake hazihamamsishi ngono kama yeye anavyosema lakini pia pamoja na kwamba mwanadada huyo amemtukana mitandaoni lakini ujumbe aliompa atakuwa ameshajifunza hata kama hataki kukubali kuwa amejifunza.

Ninachojua huyo anatafuta pa kutokea tu , maana mimi nyimbo zangu hazimaanishi ngono hata kidogo  hizo ni fikra zake na siwezi kumzua hata kidogo , mimi ninachokijua ni kwamba nyimbo zangu zinaonyesha uhalisia wa watanzania  kama zilivyo ngoma zetu.

Hata hivyo picha hiyo ambayo ilizua tafrani katika mitandao iliwezz kufutwa dakika chache na wamiliki wa mtandao wa instagram baaada ya kuripotiwa na watu kuwa haukuwa inaendana na maadili ya kitanzania.

Kwa Faiza Ally  kuweka picha za aina hii ni jambo la kawaida kwake , hii sio mara ya kwanza na haitakuwa mara ya mwisho kutokana na kauli zake anazowajibu watu wanaomshauri kutokufanya kitu hicho.

Snura Aibuka Kudai Haki Zake Mahakamani

Mwanamama anaendelea kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na uchezaji wake katika video zake na kufanya vizuri katika stage za muziki  Snura Mushi maarufu kama Snura Majanga ameibuka na kwenda mahakamani kudai haki zake za malipo kwa kampuni moja nchini baada ya kampun hiyo kutumia wimbo wake wa Majanga katika tangazo lao bila kuwa na idhini yoyote kutoka kwake kama mmiliki wa nyimbi hiyo.

Snura anasema kuwa kampuni iyo inayoshughulika na bidhaa za unga imetumia wimbo wake wa majnaga katika matangazo yao lakini yeye hakuwa na taarifa zozote kama mmiliki hiyo inabidi kampuni iyo imlipe fidia kwa kosa ilo.

Akiongezea , anasema kuwa tayari alishatafuta mwanasheria na mwanasheria huyo alishawatumia ‘notice’ kampuni hiyo ya unga kuwa ndani ya siku saba wawe tayari wameshamlipa fidia yake inayokadiriwa kuwa ni bilioni 2.1 kwa kutumia wimbo huo.

Hata hivyo Snura anasema kuwa kesi hiyo imesota kwa muda wa zaidi ya mwaka sasa na ameshaangaika sana na kutafuta wanasheria mara tatu zaidi, na alitumia baadhi ya mamalka husika na bado hakuweza kufanikiwa kwa chochote.

kwakweli nimesumbuka kwa muda mrefu sana,tangu mwaka 2015 nimetafuta wanasheria zaidi ya mara tatu  ikashindikana, na bado nilienda mpaka COSOTA  nako hakuna kilichoeleweka  lakina kwa sasa nimepata mwanasheria mwingine  ambae naamini kuwa atanifanikisha na nitapata haki zangu kama ilivyokuwa  maana ushahidi na kila kitu kipo

Snura hatokuwa msanii wa kwanza kupeleka kampuni mahakamani, hivi karibuni kulikuwa na kesi nyingine mahakani iliyohusisha kampui ya tigo na wasanii Ay na Mwana Ka kutokana na kutumia nyimbo zao kwa miito ya simu kwa wateja bila kuwa na ridhaa yao.

Makampuni na vyombo vingi vimekuwa vikitumia nyimbo za wasanii katika shuguli zao bila kuwa na hati miliki kutoka kwa msanii husika , ambapo hii ni moja ya kukandamiza na kuwaburuza wasanii kwa sababu wanapotoa ngoma zao moja ya vitu vinavyotakiwa viwape faida ni matumizi ya nyimbo hizo katika matangazo na shughuli mbalimbali za kiofisi kwa sbabu hata wao kuna faidia wanaingiza wanapotumia nyimbo hizo.

Ghafla!
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.